UREMBO BANDIA NUSURA UMUUE

Andressa Urach
Mwanamke aliyemaliza katika nafasi ya pili ya mashindano ya urembo amesema kupenda sana kujiweka urembo bandia nusura umletee mauti yake.
Andressa Urach alimaliza wa pili katika mashindano ya urembo ambapo mashabiki walimpigia mwanamke waliyehisi kuwa na makalio mazuri zaidi katika nchi yao kupitia kwenye mtandao wa internet.
Ili kujiongeza urembo, Urach aliambia jarida la Daily Mail la Uingereza kwamba alidungwa sindano za kemikali ili kufanya makalio yake kuwa makubwa pamoja na kuongeza ukubwa wa miguu yake.
Lakini mnamo mwaka 2013, mwili wake ulianza kuoza ndani.
Athari za kujiweka urembo bandia zilianza kumwandama wakati Urachhadi madaktari wakalazimika kutoa kemikali hizo kutoka mwilini mwake mwezi Novemba kwa kuchimba mashimo katika mapaja yake.
Mwili wake ilipatwa na mshtuko kwa sababu ya ugonjwa alioupata kwa kutumia vifaa chafu vya matibabu mwilini mwake.

Madaktari hata hivyo waliweza kuokoa maisha yake lakini hadi leo anatumia tu kiti cha magurudumu na miguu yake ina mashimo mwengi ambayo madaktari waliweza kutoboa ili kutoa kemikali zenye sumu alizotumia kuongeza ukubwa wa makalio na miguu.
Daktari mmoja wa kurekebisha na kutibu athari zinazotokana na urembo bandia alisema ugonjwa aliopuata Urach ulitokana vifaa chafu.
''Ninalipia makosa yangu leo kwa sababu nilitaka urembo kwa kila hali, ili nionekane kuwa kamili. Mungu ananiadhibu'' Urach aliambia Mail.
''Lakini badala ya kujiongeza urembo, niliharibu mwili wangu na sasa hata hauna sura.''

Urach pia alisema kwamba alikuwa na mazoea mabaya ya kufanyiwa uapasuaji wa kujiongeza urembo bandia kila alipojihisi kufanya hivyo.
''Sikuwahi kutafakari mara mbili wakati nilipokuwa nafanyiwa upasuaji lakini watu waliponionya nilidhani tu nitaweza kukabiliana na athari za hayo baadaye. '' Ningeweza kwenda kwa daktari, kama mfano nilivyozoea kwenda dukani na kuchagua nilichokitaka. Nilitaka watu wanitazame na kusema tu , ''wow''
Kwa sasa Urach amejitwika mzigo wa kuwatahadharisha wanawake wengine kuhusu hatari za urembo bandia.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI