MSIKILIZE HAPA MWIGULU NCHEMBA AKIZUNGUMZIA KUHUSU ESRCOW, URAIS 2015 NA KIONGOZI WA UPINZANI ANAYEMKUBALI

Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, mengi kayazungumza humu ikiwemo ishu ya kutangaza kugombea Urais, Escrow, skafu yake na pia kamtaja kingozi wa upinzani anayemvutia. Ishu ya kutamani kugombea Urais; “Hata kama ningetamani kwa kiwango gani, kama sitatimiza majukumu haya niliyopewa hakuna mtu atakayeniamini…” Rais wa awamu ya nne ameweka rekodi yake ya kutokulinda wahalifu… Ni Rais huyu huyu aliruhusu Waziri wake Mkuu ajiuzulu, ukiangalia kwenye rekodi ni Mawaziri wengi sana wameondoka. Mimi naamini anachotafuta ni hicho tu kutenda haki…” hapa alikuwa akizungumzia ishu ya maamuzi ya Rais kuhusu Escrow. Ishu ya kutangaza kugombea Urais; “Tutavuka mto tukifika mtoni..” Likaulizwa swali kuhusu ile skafu yake anayopenda kuivaa; “ni kitu kama kigumu sana kuja kupata vazi moja ambalo litavaliwa na Wamasai, Wanyakyusa, Wazanzibar nadhani ni ngumu sana. Nilichokiona kinaweza kikafaa kwa wote ni skafu, hata mtu aliyevaa kanzu anaweza akaweka skafu. Mama na yeye anaweza akaweka skafu…” Swali la kiongozi gani upande wa upinzani anamvutia; “… Zitto Kabwe, lakini kuchukua nchi bado hata yeye anajua …” Unaweza kuisikiliza sauti yote ya Naibu Waziri huyo kutoka kwenye show ya Mkasi hapa.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA