Posts

Showing posts from July, 2015

MAGUFULI ATAMBULISHWA ZANZIBAR, AAHIDI KUFUATA NYAYO ZA KARUME NA NYERERE

Image
MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema endapo akifanikiwa kuchaguliwa kuwa rais wa Tanzania, ataongoza nchi kwa kufuata nyayo za waasisi wa Taifa, Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume.   Dk. Magufuli alitoa kauli hiyo mjini Unguja, Zanzibar jana, baada kupokewa na mamia ya wananchi kwenye Uwanja wa Ndege wa Karume, huku akiwa na ulinzi mkali tofauti na siku zote.   Alisema viongozi hao waliweka misingi iliyojali kila mtu jambo ambalo limesaidia kuweka umoja, amani, utulivu na mshikamano.   “Nawahakikishia kuwa nitafuata nyayo za waasisi wetu endapo mtanipa ridhaa ya kuongoza Oktoba, mwaka huu.   “Nina deni kubwa kwenu na kwa nchi yangu, eleweni hamtajutia uamuzi wa kunichagua, nitafanya kazi kwa bidii, utii na maarifa kulijenga Taifa hili bila kumbagua mtu yeyote,” alisema Dk. Magufuli              Alisema Taifa lolote duniani linalopuuzia kujenga umoja, upendo na mshikanao

KINGUNGE AENDELEA KUMLILIA LOWASSA, ASEMA SIO FISADI KAMA ANAVYOSEMWA

Image
Mwanasiasa Mkongwe katika medani za siasa nchini Tanzania Kingunge Ngombale Mwiru ameibuka na kuzungumza na Waandishi wa Habari leo  kuhusiana na  mchakato wa kumpata mgombea Urais CCM uliopelekea jina la Mbunge wa Monduli Edward Lowassa kukatwa. Akizungumza katika mkutano huo Kingunge amesema   Kamati ya Maadili huko nyuma ilikuwa ni chombo cha kuandaa taarifa ili kuisadia Kamati Kuu katika  kuwajadili wagombea  lakini safari hii Kamati ya Maadili imefanya kazi isiyowahusu kikatiba  ikiwemo  kukata majina ya wagombea. Amesema  Kamati ya Maadili ya Chama cha Mapinduzi (CCM)  yenyewe imekosa maadili ya kuheshimu katiba na taratibu za chama kwa kujipa madaraka ya kupeleka majina 5 kwenye kamati kuu, ambayo ilipaswa kuhoji wagombea wote 38. “Kuna baadhi ya watu waliamua kuitumia Kamati ya Maadili kuandaa watu wao na kuwakata wengine kwa sababu zao.”  Amesema Kingunge. Kingunge  amedai kwamba  CCM ni chama cha wanachama wote, taratibu na kanuni zikipuuzwa na kufanya v

EMMANUEL MBASHA AKUTWA NA HATIA YA UBAKAJI

Image
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala imesema mfanyabiashara na muimbaji wa muziki wa injili Emmanuel Mbasha ana kesi ya kujibu katika shtaka linalomkabili la ubakaji linalomkabili.   Katika shtaka hilo Mbasha anadaiwa kumbaka binti mwenye umri wa miaka 17 (jina linahifadhiwa) ambaye ni shemeji yake.   Mbele ya Hakimu Flora Mjaya, mwendesha Mashtaka Munde Kalombola alidai mahakama imemkuta Mbasha na hatia baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili.   Mbasha ambaye ni mume wa muimbaji maarufu wa muziki wa injili Flora Mbasha anadaiwa kumbaka shemeji yake huyo kati ya Mei 23 na 25 mwaka huu eneo la Tabata ambako alikuwa akiishi naye.   Kesi hiyo ilianza kusikilizwa mahakamani hapo Septemba 5, 2013 ambapo binti huyo aliieleza Mahakama kuwa alibakwa na shemeji yake (Mbasha) kwa awamu mbili tofauti kabla ya kufanikiwa kukimbia.   Kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2003 sura ya 20 kifungu cha 186, kifungu kidogo cha tatu, kesi hiyo inasikilizwa n

KITUO CHA POLISI STAKISHARI KIMEVAMIWA NA MAJAMBAZI NA KUUA POLISI NAKUPORA BUNDUKI AINA YA SMS USIKU WA KUAMKIA LEO.

Image
                 

KINGUNGE ATABIRI ANGUKO LA CCM

Image
Kingunge Ngombare Mwiru, ambaye ni kada mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ametabiri anguko na mpasuko mkubwa ndani   chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, endapo chama hicho  kitaacha kumpitisha mgombea urais anayekubalika kwa wananchi wengi. Kauli hiyo imekuja mara baada ya jina la Edward Lowasa kuenguliwa kutoka majina matano  yaliyopendekezwa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (CC- NEC). Kutajwa kwa majina ya Bernard Membe, Dk. John Magufuli, Amina Salum Ali, January Makamba na Dk. Asha-Rose Migiro na Kamati kuu kwamba ndio watajadiliwa na Halmashauri Kuu (NEC), kumemfedhehesha Kingunge hata kusema,  “…hatua ya kwanza itakuwa kumweka mgombea ambaye hakubaliki ndani ya chama na hakubaliki nje ya chama. Itakuwa ni kura ya hasira.” Kingunge ametoa kauli hiyo kwa kusitasita huku akionekana kuwa na huzuni wakati akifanya mahojiano na kituo cha Azam Tv   leo mchana .   Japo Kingunge hakutaja jina la Lowassa lakini ni muungwa mkono katika mbio zake

KUTOKA DODOMA: POLISI WATUMIA MABOMU YA MACHOZI KUWATAWANYA WAFUASI WA LOWASSA

Image
Wapambe wa Mbunge  wa Monduli Edward Lowassa  hivisasa wanafanya maandamano makubwa nje ya ofisi za CCM hapa makao makuu ya CCM wakipinga Mbunge huyo kuchujwa katika tano bora. Wapambe hao wanaimba nyimbo mbalimbali za kukiponda chama cha Mapinduzi kwa madai kuwa chama hicho  sio cha kindugu  na  pia  sio cha kifalme. Kwa namna nyingine  hali si shwari hapa mkoani Dodoma ambapo sintofahamu imetawala kuhusiana na Edward Lowassa kukatwa. Bado haijulikana nini hatma ya kikao kinachoendelea hivisasa kwa kuwa wa wajumbe wengi wa napinga Lowassa kuchujwa. Baishara zasimama,makao makuu Dodoma. Baadhi ya wapambe wa Lowassa wakipinga Kamati kuu kumchuja Lowassa. Barabara zafungwa Polisi watanda kila kona kudhibiti usalama dhidi ya waandamanaji. Wapambe wa Loawssa wakipinga kukatwa tano bora.

DODOMA KIMENUKA TAZAMA KIPANDE CHA VIDEO HAPA

Image

MBASHA AFURAHIA UNABII WA GWAJIMA KUTOTIMIA, ADAI ALIMUHARIBIA FAMILIA YAKE

Image
Hapa ni baadhi ya mazungumzo yake na watu wa kwenye group Wahtsaap la imani ya washindi 

MGOMBEA URAIS WA UKAWA KUWEKWA HADHARANI MUDA WOWOTE KUANZIA SASA

Image
Hatimaye leo wabunge wote wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wanakutana na viongozi wao  kumchagua mgombea urais atakayeviwakilisha vyama hivyo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.    Mkutano huo wa wabunge umekuja baada ya vikao kufanyika mfululizo wiki hii, huku kukiwa na mvutano kuhusu nani au chama gani kisimamishe mgombea urais.   “Tumeshakubaliana namna ya kugawana kata na majimbo 13 yaliyobaki na Jumamosi tutaweka wazi kwa wananchi. Pamoja na hilo pia tutamtangaza mgombea urais na chama anachotoka,”  alisema Dk Makaidi  jana.   Umoja huo umekuwa ukiongezeka nguvu tangu wakati wa mchakato wa Katiba mwaka jana, hali inayosababisha wafuasi wake kuamini kuwa yeyote atakayesimamishwa na umoja huo na kupigiwa kampeni kwa pamoja anaweza kujikuta anakuwa rais, mbunge au diwani.   Mvutano Vikao vya umoja huo vilitawaliwa na mvutano baina ya wajumbe ndani ya umoja huo hasa katika nafasi ya mgombea urais baada ya kuwapo kwa watia nia zaidi ya mmoja.  

EDWARD LOWASSA KUKATWA: NCHIMBI, SOPHIA SIMBA NA ADAM KIMBISA WAPINGA

Image
Habari kutoka makao makuu ya CCM mkoani Dodoma  ni kwamba wajumbe wa kamati kuu  watatu ambao ni  Dkt. Emmanuel Nchimbi, Sophia Simba na Adam Kimbisa  wamepinga maamuzi ya kamati ya kumkata mmoja wa wagombea maarufu   na kumweka mgombea asiyekuwa maarufu.   Akizungumza usiku huu majira ya saa saba za usiku Dkt. Nchimbi amesema kwamba wao watatu hawajakubaliana na maamuzi ya kamati kuu iliyoketi usiku huu chini ya Mwenyekiti Dkt Jakaya Kikwete kumkata mgombea maarufu kwa manufaa ya mgombea asiye maarufu.   “Katika kikao cha leo kamati haikupoea majina yote yaliyojadiliwa na maadili, suala ambalo ni kinyume na kanuni, pili katiba ya CCM inataka mtu anayekubalika  ndiye apewe nafasi ya kwanza, lakini kikao cha leo kimeonyesha kuminya wanaokubalika  kwa manufaa ya wachache wasiokubalika”  Amesema Dkt. Nchimbi.   Hivyo basi kwa sababu hiyo wao watatu ambao ni wajumbe wa kamati kuu wamewataarifu wenzao  kwamba wamejitenga na maamuzi ya kikao hicho na kutangaza kuto kuyaunga

CCM YAPITISHA MAJINA MATANO YA WAGOMBEA;LOWASSA HAYUMO

Image
Kikao cha Kamati Kuu ya chama cha mapinduzi (CC) kimemalizika hivi punde(saa saba usiku)  mjini Dodoma. Tovuti ya CCM imeyatangaza majina matano yaliyopitishwa na Kamati ya CCM (CC) kuwa ni ; 1) Bernard Membe 2) John Magufuli 3) Asha Rose Migiro 4) January Makamba 5) Amina S. Ali

KIKWETE APANGUA VIKAO VYA KAMATI YA MAADILI

Image
WAKATI Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, akipangua ratiba ya vikao muhimu vya Kamati ya Usalama na Maadili pamoja na Kamati Kuu vilivyotarajiwa kufavyika jana na leo, Mwanasiasa maarufu, Kingunge Kombale-mwiru leo alikuwa uso kwa uso na Katibu Mkuu wa chama hicho katika jitihada za kumuokoa Edward Lowassa. Katika siku ya leo kulikuwe na minong’ono ya hapa na pale iliyokuwa imeenea katika korido za Makao Makuu ya CCM na viunga vya mji wa Dodoma, ikidai kuwa jina la mwanasiasa huyo halitakuwemo katika orodha ya majina ya tano bora itakayopelekwa ndani ya NEC kutoka Kamati Kuu. Minong’ono hiyo ya kuwepo uwezekano wa jina la Lowassa kutotoka Kamati Kuu, iliongeza hofu zaidi miongoni mwa wapambe wa mwanasiasa huyo, baada ya mwanasiasa mkongwe nchini anayejulikana wazi kuwa katika kambi ya mgombea huyo, Kingunge Ngombale-Mwiru kutinga katika Ofisi za Makao Makuu ya chama hicho mchana wa kati ya saa 8:00 na saa 9:00. Baada ya kushuka kwenye gari

HOTUBA YA RAIS YA KUAGANA NA WABUNGE NA KULIVUNJA BUNGE LA 10 LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Image
Mheshimiwa Spika; Tunayo kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma kwa kutujalia uzima na kutuwezesha kuishuhudia siku hii adhimu katika historia ya Bunge letu na nchi yetu. Hatimaye siku ya kuvunja Bunge la Kumi imewadia ili kuwezesha hatua husika za mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ziweze kutekelezwa. Nakushukuru sana Mheshimiwa Spika kwa kunipatia nafasi hii ya kulihutubia Bunge lako tukufu ili niweze kutimiza wajibu wangu huo wa msingi Kikatiba. Lakini, shukrani zangu kubwa ni kwa uongozi wako mahiri na shupavu. Umeliongoza Bunge vizuri. Najua haikuwa kazi rahisi. Penye wengi pana mengi. Lakini kwa uhodari mkubwa umeweza kulifikisha jahazi bandarini salama salmini. Hakika wewe ni nahodha makini na jemedari hodari, uliyethibitisha uhodari na umakini wako katika uwanja wa medani. Wewe ndiwe mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huu wa juu kabisa katika mhimili huu wa kutunga sheria na umeidhihirishia dunia kuwa wanawake wakipewa nafasi wanaweza. Mheshimiwa S