Posts

Showing posts from November, 2014

MAGAZETI YA LEO YAKISOMWA LIVE

HAYA HAPA MAJINA YALIYOTEULIWA NA PAC KUANDIKA MAAZIMIO YA KUWAWAJIBISHA WATUHUMIWA WA ESCROW

Image
Baada ya Spika wa Bunge kuahirisha Bunge mara mbili siku ya leo Novemba 29 ili kuipa nafasi kamati ya PAC iweze kufanya marekebisho ya maneno yaliyoandikwa kwenye maazimio yaliyowasilishwa na Kamati ya PAC, Mwenyekiti wa Kamati hiyo  Zitto Kabwe  ametaja majina ya walioteuliwa na Kamati hiyo kuandika maazimio ya kuwajibisha watuhumiwa wa Tegeta Escrow. Kupitia ukurasa wake wa Facebook (@ Zitto Kabwe ) ameandika majina ya wajumbe hao.

IKULU YAHUSISHWA NA ESCROW

Image
       Ikulu Bunge la Tanzania hapo jana liliambiwa kwamba afisa mmoja wa ikulu ya rais bwana Prosper Mbena aliandika barua ili kushinikiza hatua ya kutolewa kwa billioni 306 fedha za Escrow kutoka banki kuu ya Tanzania. Bwana Mbena ambaye anafanya kazi kama katibu katika afisi ya rais aliandika barua mwaka uliopita akiiagiza wizara ya fedha kuzitoa fedha hizo kama ilivyoamrishwa na mwanasheria mkuu. Kushirikishwa kwa ikulu ya ya rais kulizuka baada ya wabunge kujadili ripoti kuhusu kashfa hiyo ambayo imeikumba serikali ya Tanzania katika miezi kadhaa iliopita. Kiongozi wa upinzani katika bunge,Bwana Freeman Mbowe pamoja na kinara wa bunge upande wa upinzani bwana Tandu Lissu alifichua jukumu lililochukuliwa na afisa huyo wa ikulu kushinikiza madai kwamba baadhi ya maafisa wakuu serikalini walihusika katika utoaji wa mabilioni hayo ya fedha. Ripoti hiyo imesema kuwa fedha hizo za Escrow ni za walipa ushuru wa Tanzania na kwamba zilitolewa kwa njia ya ufisadi na kugawanywa mi

BREAKING NEWS; HELKOPTA YA TANAPA YAPATA AJALI MAENEO YA KIPUNGUNI

Image
Helikopta ya Maliasili (TANAPA) imedondoka maeneo ya Kipunguni, jijini Dar na kuua watu wote watano wakiwemo rubani na Polisi. Kwa taarifa zaidi tutazidi kukufahamisha

MAGAZETI YA LEO TAREHE 28/11/2014

Image
. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .    

PROF MUHONGO; FEDHA ZA ESCROW SI MALI MALI YA UMMA

Image
Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo Dodoma.  Sakata la uchotwaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow linaendelea kuchukua sura mpya baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo kutoa ufafanuzi wa Serikali bungeni mjini Dodoma kuwa fedha hizo si za umma na kwamba bado Serikali ina mzigo wa madeni katika sakata hilo. Kauli ya Prof Muhongo inakuja siku moja baada ya Kamati ya PAC kuwasilisha ripoti yake jana juu ya suala hilo ambapo pamoja na mambo mengine, Kamati ya PAC ilijiridhisha kuwa sehemu ya fedha hizo ni za Serikali. Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe akisoma taarifa ya kamati hiyo jana alisema Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Francis Mwakapalila, Kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bade wakithibitisha kuwa sehemu ya fedha zilizokuwamo kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow zilikuwa za Serikali. Akiwasilisha maelezo ya Serikali leo, Prof Muhongo alipangua hoja moja baada ya nyingine zilizotolewa na Kamati ya PAC

WATU 11 WAFA AJALINI MKANYAGENI TANGA

Image
WATU 11 wanadaiwa kufariki dunia huku wengine wakijeruhiwa katika ajali mbaya eneo la Mkanyageni mkoani Tanga baada ya gari aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T 410 BJD kugongana na Scania namba T 605 ABJ asubuhi hii. Katika ajali hiyo, Coaster lilikuwa likitoka mkoani Tanga kwenda Lushoto na madereva wa magari yote mawili hawajulikani walipo baada ya ajali. Miili ya marehemu katika ajali hiyo imehifadhiwa katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Muheza, Tanga. Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi. AMEN

Baada ya ishu ya Escrow, haya ni majibu mawili ya Waziri Mkuu Pinda ikiwemo kujiuzulu

Kikao cha Bunge leo Novemba 27 kimeanza kwa maswali mawili kuulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni  Freeman Mbowe  kwa Waziri Mkuu  Mizengo Pinda . “ …Chini ya uongozi wako kama Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ukiwa kiongozi wa shughuli za Kiserikali Bungen, tumeiona Serikali ikikumbana na matatizo na vikwazo vingi ikiwemo ‘Operesheni Tokomeza’ ambayo ilipelekea wananchi wengi kupoteza maisha na wengine kupata vilema… “–  Mbow e. Tumeona mauaji ya raia yakiendelea Kiteto, kashfa kubwa ambayo iko current sasa hivi ikiwa ni pamoja na kauli zako ulizowahi kuzisema kwamba fedha zilizopotea za akaunti ya Escrow hazikuwa fedha za umma bali zilikuwa fedha za watu binafsi… “–  Mbowe . Baada ya Ripoti ya CAG kutolewa hadharani kuhusiana na fedha za Escrow na baada ya Ripoti ya PCCB kutolewa na hatimaye jana hapa Bungeni kusomwa taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, nini msimamo wako kuhusu kauli yako ya awali kwamba fedha zile zilikuwa ni za watu b

AJALI YA MPAKANI MWA ZAMBIA NA CONGO, TAHADHALI PICHA ZA KUTISHA

Image
Magari makubwa yakiwaka moto baada ya moto huo kuzuka maeneo ya Kasumbalesa, mpakani mwa  AJALI mbaya ya moto imetokea juzi majira ya saa kumi na moja jioni maeneo ya Kasumbalesa, mpakani mwa Zambia na Kongo baada ya lori moja kulipuka kwa moto na kuchoma malori mengine yaliyokuwa jirani yake. Inadaiwa magari mengi yameungua yakiwemo kutoka Tanzania japo idadi kamili ya maafa yaliyotokana na ajali hiyo bado hayajafahamika.

HII HAPA NDIO RIPOTI YA PAC ILIYOSOMWA LEO JIONI

Image
Mwenyekiti wa kamati ya hesabu za serikali(PAC) Zitto Kabwe Mwenyekiti wa kamati ya hesabu za serikali(PAC) amewasilisha ripoti ya sakata ya Escrow katika mkutano wa 16/17,kikao cha 17 bungeni Dodoma. ZITTO: Kamati imebaini kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa barua yenye Kumb Na. AGCC/E.080/6/70 ya tarehe 18 Novemba, 2013 alimthibitishia Gavana kuwa hakukuwa na kodi ya Serikali katika fedha zilizokuwa kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW na kwamba fedha hizo zihamishiwe IPTL ili Serikali ijinasue na mashauri yasiyo na tija kwake. Kutokana na mahojiano kati ya Kamati na Kamishina Mkuu wa TRA ilibainika kwamba Kampuni ya Piper Links haijulikani sio tu British Virgin Islands bali hata nchi nyingine.  Kamati haielewi ni jinsi gani taasisi kubwa kama Benki Kuu ya Tanzania, Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Fedha, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na nyingine zilizohusika katika suala hili, na ambazo tunaamini zimesheheni Watendaji wenye weledi, zimewezaje. Wakati mahojiano ya Kam