VURUGU BUNGENI ZASABABISHA BUNGE KUAHIRISHWA LEO




Baada ya Mbatia kuleta hoja ya dharura juu nguvu iliyotumiwa na polisi kwenye maandamano ya CUF jana tarehe 27 January ili ijadiliwe na wabunge kama hoja ya dharura, spika Makinda aliamuru serikali ilete majibu kesho ndio ijadiliwe. 

Wabunge walisimama kushinikiza hoja ijadiliwe lakini Makinda aliendelea na msimamo wake wa hoja kujadiliwa kesho baada ya Serikali kuleta majibu, hapo ndipo sintofahamu ilipozidi na kuleta kutoelewana kati ya wabunge wa Upinzani na Spika. Ilibidi spika Anna Makinda kuahirisha bunge mpaka kesho lakini baadae akabadili na kusema saa kumi jioni leo hii.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI