Posts

Showing posts from September, 2014

MAGAZETI YA LEO KURASA ZA MBELE NA NYUMA

Image

MAGAZETI YA LEO KURASA ZA MBELE NA NYUMA

Image

KIONGERA KUTIBIWA NJE YA NCHI

Image
                                  Patrick Kiongera            Daktari maarufu wa michezo ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema kuwa kunauwezekano mkubwa Simba ikalazimika kumpandisha Ndege mshambuliaji wake Paul Kiongera akatibiwe.             Daktari huyo amesema kama Kiongera anaugonjwa sugu wa goti ni vigumu sana kunusurika kufanyiwa upasuaji ''ugonjwa wa goti unamambo mengi siwezi kusema kila kitu kwa kuwa majibu ya            Kiongera sijayaona, Kama ni ugonjwa sugu asilimia kubwa ni upasuaji na mara nyingi ni nje ya Nchi'' alisema daktari huyo bingwa.         Kiongera alikaa nje kwa wiki sita ambao ni muda wa wiki mbili na nusu, hata hivyo majibu ya daktari aliyempima ndio yaataamua wapi akatibiwe. Kiongera aliumia katika mechi dhidi ya Coastal Union akiwa ameingia kuchukua nafasi ya Amissi Tambwe

TAMBWE; TUMEELEWANA NA OKWI SUBIRINI MOTO WETU

Image
                     Mshambuliaji wa Simba kinara wa mabao ya ligi kuu Bara Ammisi Tambwe                        Emmanuel Okwi mshambuliaji  hatari wa Simba           Mshabuliaji wa Simba raia wa Burundu Amissi Tambwe amesema anafurahia ushirikiano wake na Emmanuel Okwi katika kikosi cha na kuahudi kuwa watafanya makubwa katika mechi zijazo. Kauli ya Tambwe imekuja kabla ya Simba kuivaa Polisi Moro katika Ligi kuu Bara kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini.         Tambwe alieleza kuwa amefurahi kuona amefunga katika mchezo wa kwanza wa Ligi kuu Bara na kumwagia Sifa Okwi kwa uwezo ''Tumecheza vizuri na Okwi ni mchezaji tunaeelewana vizuri .Naamini tutafanya vizuri zaidi hapo mbele  Lengo ni kuhakikisha tunaitumikia vizuri timu yetu na kuona inafanya vizuri msimu huu'' alisema Tambwe.

MGOSI; JAJA AKIZOEA BONGO ATAKUWA HATARI

Image
         Straika wa Yanga Mbrazil Geilson Santana 'Jaja               Straika wa timu ya Mtibwa Sugar ya Mkoani Morogoro, Mussa Hassan Mgosi amemtabiria makubwa straika wa Yanga, Mbrazil Geison Santana 'Jaja' kwa kusema atakuwa mchezaji mzuri pindi atakapozoea mazingira ya Tanzania na viwanja vyake.       Jumamosi iliyopita Mgosi aliifungia timu yake bao moja katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga, huku Jaja akishindwa kufunga na na kukosa Penalt.      Mgosi alisema Jaja ni mchezaji mzuri ila bado hajazoea viwanja vya Tanzania ndio maana anapata wakati mgumu.Anahitaji kuzoea mazingira ya viwanja vyetu vya Tanzania ndipo aweze kufanya vizuri.

ALIVYOFANYIWA MESSI BARCA IKILAZIMISHWA SULUHU

Image
  Beki wa Malaga, Weligton akimkwida mashavuni nyota wa Barcelona ,Lionel Messi kabla ya kumsukuma chini hadi akapewa kadi ya njano na Refa Alejandro Hernandez, timu hizo zilitoka sare bila kufungana katika mchezo wa La Liga usiku wa kuamkia leo. Lionel Messi baada ya kusukumwa na na beki wa Malaga,Weligton.

MECHI YA SIMBA,YANGA OCTOBA 12 YAAHIRISHWA.

          Ile mechi ya Yanga dhidi ya Simba imesogezwa mbele na TFF haijasema itakuwa siku gani.Badala yake siku hiyo kutakuwa na mechi ya Taifa Stars.Timu ya Taifa, Taifa Stars itashuka uwanjani octoba 12 mwaka huu kuikabili Benin katika Mechi ya kirafiki ya kalenda shirikisho la Kimataifa la mpira wa Miguu FIFA       Mechi hiyo itachezwa uwanja wa Taifa Dar es salaamkuanzia saa kumi kamili jioni.Program ya Taifa Stars inayodhaminiwa na na Kilimanjaro premium Lager kwa ajili ya mechi hiyo itatangazwa na na kocha mkuu Mart Nooij.       Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania linaendelea na taratibu nyingine kwa ajili ya mechi hiyo ikiwemo usafiri wa Benin kuja nchini ambapo timu hiyo inatarajiwa kutua Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Oktoba 10 mwa huu ikiwa na msafara wa watu 28.       Pambano la Stars na Benin litatanguliwa na mechi ya kudumisha upendo kati ya viongozi wa dini ya Kiislam na Kikristo.       Wakati huo huo  kutokana na mechi hiyo ratiba ya Ligi Kuu ya Vo

RASIMU YA WARIOBA VS SITTA

Image

JAJA ASHAURIWA KUONDOKA NCHINI

Image
        Klabu ya mtibwa Sugar imesema kuwa Straika wa Yanga Mbrazili Geilson Santos 'Jaja' atachemka katika ligi ya Bongo na kusisitiza ingekuwa busara kama wangemuandalia mapema nyaraka zake ili arejee kwao kuendelea na majukumu mengine.         Kitendo cha Yanga kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Mtibwa juzi jumamosi kwenye uwanja wa jamhuri, Morogoro kimeendeleza 'uteja' wa timu hiyo katika uwanja huo kwani kwa mara ya mwisho Yanga kuibuka na ushindi katika timu hiyo ilikuwa ni Septemba 19,2009.ikiwa chini ya kocha Dusan Kondic.        ''Tumeanza kuibabua Yanga na Jaja wao maana kila mara ilikuwa ni Jaja, Jaja Jaja huyo Jaja ndio nani? amefichwa na mabeki imara hakuonekana kabisa uwanjani''walisema.        Waliongeza kuwa Jaja ni ni Straika mwenye umbo zuri,na siyo uwezo uwanjani unajua timu zetu hizi zinaamini watu kutoka nje kuliko vijana wa hapa kitu ambacho si sahihi.

ALIPA MILIONI 33 KUONGEZEWA TITI LA TATU

Image
                                Justimine Tridevil katika pozi                            Mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Justimine Tridevil mwenye umri wa miaka 21 amedai kufanyiwa upasuaji na kuongezewa titi la tatu kupitia mahojiano aliyoyafanya Redioni.          Justimine ambaye ni raia wa Tampa Jijini Florida Nchini Marekani anayejishughulisha na huduma ya Massage alilipa kiasi cha dola za Marekani 20,000 sawa na mil. 33.4 za Tanzania kufanyiwa upasuaji huo.          Mwana mama huyo katka mahojiano ya Real Radio 104.1 ameamua kufanya hivyo ili asiwe na mvuto kwa wanaume maana hataki na mpenzi huku akitaka kuwa staa katika TV japo alipoulizwa kwa nini hataki kuwa na mwenza hakutaja sababu.          Takribani miaka 50 walikataa kumfanyia upasuaji huo wakiogopa kuvunja ya fani yao hivyo kumchukua miaka miwili kupata Daktari aliyekuwa tayari kufanya hivyo.Kwasasa mwanamke huyo anarekodi video itakayomuonyesha changamoto atazokutana nazo akiwa mwanamke mwenye matiti mat