SSERUNKUMA ACHEZA DAKIKA 500 BILA BAO



                             Dan Sserunkuma
STRAIKA wa Simba, Dan Sserunkuma, bado anasotea bao lake la kwanza katika mechi za mashindano mpaka sasa ambapo hesabu zinaonyesha amecheza zaidi ya dakika 500 bila kucheka na nyavu.
Sserunkuma ambaye tangu atue Msimbazi mwishoni mwa mwaka jana akitokea Gor Mahia ya Kenya, amecheza mechi moja ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar ambapo Simba ilichapwa bao 1-0.
Baada ya mchezo huo mshambuliaji huyo raia wa Uganda aligeukia katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi ambapo katika mechi za hatua ya makundi alicheza zote huku akikosa kufunga zikiwemo mechi mbili za hatua ya robo fainali na nusu fainali.
Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic, alisema anatambua kwamba Sserunkuma bado hajaifungia Simba, lakini bado ana imani kubwa na mshambuliaji huyo.
“Nikweli unapozungumzia mshambuliaji ni lazima uone anafunga, lakini hali hii haiwezi kuwa ngeni kwa Dan (Sserunkuma) bado nina imani kubwa naye naamini atarudi katika ubora wake,”alisema Kopunovic amabaye anaamini hali hiyo ni sehemu tu ya mchezo.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI