PROF. LIPUMBA,VIONGOZI WAANDAMIZI NA WANACHAMA - WAMEACHIWA KWA DHAMANA



Viongozi na wanachama wote waliokuwa wameshikiliwa hapa CENTRAL POLICE wameachiwa kwa dhamana na kukabidhiwa vifaa vyao walivyosalimisha awali. Kuripoti tena ni leo saa 4.00 asubuhi.
Shukrani za dhati ziwaendee mawakili wa CUF akiwemo wakili msomi Hashim Bakari Mziray na wakili mzoefu Job Krario.
Pia shukrani kubwa ziwaendee mawakili wengine wawili walioletwa na CHADEMA na mmoja wa NCCR.
Tukio hil limeonesha kuwa UKAWA inafanya kazi kama siafu. Mawakili wengine watatu walikuwa njiani kuja hapa CENTRAL tumewarudisha, jumla wangekuwa saba.
Kwa uwezo wa mungu HAKI itapatikana siku moja Tanzania. Mabadiliko ni mimi, wewe na yule na yanaanza sasa na yanaanzia kwako na kwangu na kwa yule.
Mimi na wewe ndiyo tunawakilisha Tanzania tuitakayo, tuanze sasa na tuendelee kuiunga mkono UKAWA na juhudi zake.
Kwa dhati pia niwapongeze Katibu Mkuu wa NCCR, Mosena Nyambabe, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, Mkurugenzi wa Fedha wa CUF Joram Bashange, Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu CUF Mhe. Kuruthum Mchuchuli (MP), Mjumbe wa Baraza Kuu CUF Bonifasia Mapunda na Mjumbe wa Baraza Kuu mstaafu Maharagande Mbarala kwa kuwepo CENTRAL POLICE hadi sasa.
Niwapongeze viongozi na wanachama wote waliosimama kidete hadi usiku, malipo yenu ni kupatikana kwa Tanzania tuitakayo.
Mungu awabariki na usiku mwema.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI