MBWANA SAMATTA AKIWA KWENYE MAZOEZI HISPANIA NA CLUB YA RUSSIA.

Mbwana Samatta majaribioni CSKA Moscow Jan 21 2015Mwandishi wa habari za michezo Tanzania Shaffih Dauda ameripoti kwamba staa wa soka kutoka Tanzania Mbwana Samatta ambaye anachezea club ya TP Mazembe, Congo DRC yuko nchini Hispania sasa hivi kwa ajili ya kufanya majaribio ya soka la kulipwa na club ya CSKA Moscow ya Russia ambayo kwa miaka kadhaa imekuwa ikitawala soka la nchi hiyo na kucheza katika michuano ya mabingwa wa Ulaya.
Mbwana 2
Samatta alipewa nafasi ya kufanya majaribio ya siku 3 na klabu hiyo kwenye kambi yao ya mazoezi iliyopo Spain, lakini ameongezewa wiki moja ya ziada ili maofisa ya jopo ya ufundi la timu hiyo wapate muda wa kumuangalia vizuri.
Katika moja ya mechi za majaribio alizoichezea CSKA, Mbwana tayari amefunga magoli mawili.
Mbwana 3
Mbwana 4

Mbali ya Samatta kufanya vizuri katika mazoezi hayo, club hiyo kwenye ukurasa wa Facebook imesema hawana mpango kufanya usajili wa mchezaji huyo kwa sasa; “PFC CSKA trial for Mbwana State Tanzanian striker Mbwana State is currently on trial with PFC CSKA. He’s currently training with the team. “State will take part in one of the two upcoming friendly matches,-our manager Leonid Slutsky told pfc-cska.com. -However, we will not be signing him. “#CSKAforever
CSKA Moscow

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA