MBIO ZAMUOKOA MUAMUZI UWANJANI



MBIO za mwamuzi, Ezekiel Ngoji, wa Shinyanga juzi Jumapili zilimwokoa asipate kipigo cha nguvu kutoka kwa wachezaji wa Polisi Dodoma baada ya kutokea vurugu kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza dhidi ya Toto African katika Uwanja wa Kirumba jijini hapa.
Vurugu hizo ambazo zilifanya Polisi waliokuwepo uwanjani hapo kufyatua mabomu ya machozi kadhaa kuthibiti hali hiyo.
Awali mchezo ulianza vizuri lakini hali ilibadilika kipindi cha pili kwenye dakika ya 63 baada ya mwamuzi Ngoyi kutoa penalti kwa Toto kwa kile kilichoelezwa kipa wa Polisi Madopi Mwingira alimchezea rafu mmoja wa washambuliaji wa Toto.
Penalti hiyo ilipigwa na Hamim Abdul ambaye alifunga na sekeseke lilianza baada ya mwamuzi huyo kumtoa kwenye benchi mmoja wa makocha wa Polisi na ndipo vurugu hizo zilipoanza kwa mmoja wa wachezaji wa Polisi kuanza kumshambulia mwamuzi Ngoyi.
Baada ya kuona hivyo mwamuzi huyo alitimua mbio kuelekea jukwaa kuu kujiokoa na kipigo hicho hali iliyowafanya askari waliokuwepo uwanjani hapo kufyatua mabomu ya machozi kuzuia vurugu hizo.
Dakika 20 baadaye, waamuzi hao walitoka jukwaa kuu wakiwa na maofisa wa Polisi na viongozi wa Chama cha Soka Mkoa wa Mwanza(MZFA)na kwenda uwanjani kupiga kipenga cha kumaliza pambano.
Kocha wa Polisi Dodoma, Gabriel Marwa alisema mwamuzi wa mezani ndiye aliyeharibu pambano kwa kuwatoa bila sababu kwenye benchi viongozi wenzake jambo lililosababisha hali hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI