BOSI ALIYEBEBWA ILI VIATU VISIHARIBIKE KWENYE BARAFU AACHISHWA KAZI

Mr. Ofisa II

Nedim Zunarci akiwa amebebwa

Picha zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii Uturuki zikimuonyesha kiongozi wa Idara ya Huduma Vijijini akiwa amebebwa juu na wakulima ili kukwepa barafu zilimponza, ikaamriwa asimamishwe kazi.
Afisa huyo, Nedim Zunarci alionekana amebebwa na wakulima hao katika Jimbo la Manisa wakati akikagua athari zilizosababishwa na barafu aliyoanguka kutokana na baridi kali, akahofia viatu vyake vitaharibika kutokana na barafu hiyo, hivyo akabebwa na wakulima hao.
Meya wa Manisa, Cengiz Ergun alisema kitendo hicho hakiendani na utaratibu wa kazi wala maadili, pia hakionyeshi uhusiano mzuri kati ya viongozi na jamii.
Comments za watu kwenye mitandao ya kijamii Uturuki walionekana kukosoa pia kitendo hicho baada ya picha hiyo kuzagaa.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI