BEKI KING'NG'ANIZI ANAYEAMINIWA SIMBA



UNAPOZUNGUMZIA mabeki wa kati wenye uwezo mkubwa kwenye Ligi Kuu Bara, lazima awepo Salim Mbonde wa Mtibwa Sugar.
Mbonde ni chipukizi mwenye umri wa miaka 21 na juhudi zake uwanjani ndizo zimefanya jina lake litambulike kwa haraka kwenye soka nchini, sasa ni kati ya mabeki ghali Tanzania.
Mbonde amejaliwa umbo kubwa lililojengeka kimichezo na ni mrefu achezapo soka hutumia akili na nguvu kama ilivyo kwa mabeki wengine.
Sh15 Milioni zitamng’oa Mtibwa
Nyota huyo alianzia mbali kusaka mafanikio na sasa hali ya kijana ni tofauti. Hata hivyo licha ya kusogelea malengo yake bado anaendelea kutafuta.
Anafahamu maisha magumu aliyopitia na sasa anajitambua na anajiamini na huenda elimu aliyoipata inamsaidia kupanga na kufanya maamuzi sahihi.
Kabla ya kuanza kwa msimu huu, klabu kadhaa zilimuhitaji lakini kutokana na kujitambua kwake kwenye makubalino ya maandishi, ametamka kuwa timu itakayotaka kumng’oa kwenye kikosi cha Mtibwa lazima ijiandae katika dau la usajili.
Atasaini makataba kwenda timu nyingine kwa dau lisilopungua Shilingi 15 milioni ingawa kwa sasa katika timu yake ya Mtibwa anacheza kwa fedha ambayo ni chini ya hapo.
“Maisha ni malengo, kama unavyojua maisha ya soka ni mafupi ukicheza hapa mwanzoni baadaye itakuwa shida,” anasema Mbonde ambaye alianza soka katika timu yake ya mtaani ya Uhuru Rangers ya Morogoro na baadaye akajiunga na akademi ya Moro Youth chini ya makocha Hussein Mau na Alan Figo, hapo alicheza kwa miaka mitatu na kwenda JKT Oljoro na baadaye Mtibwa.
“Malengo yangu ni kucheza mpira wa mafanikio ndiyo maana napambana na habari za usajili wapo wanaohama na baadaye wanakuja kujutia.
“Naweza kucheza timu yoyote lakini nimejipangia dau la usajili, nitasajili timu nyingine kulingana na makubalino. Nitaondoka Mtibwa kama nikipewa Sh15 milioni ingawa kwa Mtibwa naweza kusaini chini ya hapo.
“Nasema hivyo kwa sababu naiheshimu Mtibwa, imenitoa mbali, nina amani ninaishi vizuri, napata kila kitu.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI