Posts

Showing posts from February, 2015

ANNA TIBAIJUKA, ENDREW CHENGE NA WILLIAM NGELEJA WASIMAMISHWA UJUMBE HALMASHAURI KUU- NEC

Image
KAMATI KUU ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo tarehe 28/8/2015, kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa kumi na moja alasiri, kimeazimia yafuatayo; > Kamati Kuu imepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, msanii wa Chama na Kada wa muda mrefu Mheshimiwa John Damian Komba. Mwenyekiti wa CCM, Mhe Dr Jakaya Mrisho Kikwete ameelezea kuwa msiba huo ni pigo kubwa kwa Chama hasa katika wakati huu wa kuelekea kwenye uchaguzi na pengo ambalo ni vigumu kuliziba. CCM imepata pigo na Kamati Kuu chini ya Mwenyekiti inatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa Kapteni John Damian Komba. Kazi yake kubwa ndani ya Chama itaandikwa katika historia iliyotukuka ya Chama Cha Mapinduzi. > Pia, kutokana na Kikao cha Kamati Kuu iliyopita iliyoiagiza kamati ya maadili kuwaita na kuwahoji wanachama na viongozi watatu waliotajwa kuhusika na kashfa ya Escrow. @ Mheshimiwa Anna Kajumulo Tibaijuka @ Mheshimiwa William Mganga Ngeleja @ Mheshimiwa Andrew Ch

TUJIKUMBUSHE NA VIDEO HII CAPTAIN JONH KOMBA AKIWA KAZINI

Image

CAPTAIN JOHN KOMBA AFARIKI DUNIA

Image
Mbunge wa Mbinga magharibi captain John Komba amefariki leo katika Hospitali ya TMJ Mikocheni jijini Dar es salaam Kwa Mujibu wa mtoto wa M arehem Bw. Jerry Komba amesema kifo cha baba yake kimetokana na ugonjwa wa kisukari ambapo alisema sukari ilishuka gafla akiwa nyumbani kwake Mbezi Beach jijini Dar.  Mbunge huyo alikimbizwa katika Hospitli ya TMJ ambapo mauti yalimkuta . Marehemu amehamishiwa katika hospitali ya Lugalo ambapo Ratiba ya mazishi bado haijafahamika.  Mungu ailaze Roho ya marehemu mahali pema peponi AMEN.

UTETEZI WA PROFESA ANNA TIBAIJUKA AKIHOJIWA NA BARAZA LA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA DHIDI YA MASHTAKA YANAYOMKABILI

Image
BARAZA la Maadili ya Viongozi wa Umma, limemsomea rasmi mashitaka aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka (pichani), na kubainisha kuwa kiongozi huyo anastahili kujibu mashitaka kwa kosa la kuomba na kujipatia fedha kinyume na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Hata hivyo, Profesa Tibaijuka alikana mashitaka hayo, na kusisitiza kuwa hakukiuka maadili hayo ya viongozi wa umma, kwa kuwa fedha hizo hakuziomba kwa maslahi yake binafsi, bali kwa ajili ya kuendeleza na kuboresha taasisi yake inayotoa huduma ya elimu kwa watoto wa kike wasio na uwezo lakini wenye vipaji. Akimsomea mashitaka hayo mbele ya baraza hilo, Mwanasheria wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Wemaeli Mtei alisema Profesa Tibaijuka ambaye ni kiongozi wa umma, alishawishi na kuomba fedha na baadaye kupokea Sh bilioni 1.6 kutoka kwa James Rugemalira na mkewe. Aidha, Sekretarieti hiyo kupitia shahidi wake ambaye ni Katibu Msaidizi wa Idara ya Viongoz

KINYESI CHA MWALIMU WA KIBASILA CHATEKETEZWA

Image
Manispaa ya Temeke leo imeteketeza kinyesi kilichokutwa katika chumba cha mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kibasila Gaudensia Albert baada ya maofisa wa afya wa manispaa hiyo kuchukua hatua hiyo ili kunusuru afya za wakazi wa eneo hilo. Kazi hiyo ilifanyika majira ya saa tisa alasiri katika eneo la Yombo, Kisiwani Kata ya Sandari jijini Dar es chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi na wakishirikiana na Mwanyekiti wa Mtaa huo, Yahya Bwanga. Akizungumza na wandishi wa habari jijini wakati wa zoezi hilo, Ofisa Afya wa Manispaa ya Temeke, Floyd Tembo alisema tukio hilo walilipata juzi juzi jioni, baada ya kulipata waliwatuma Watendaji wa Afya wa Kata hiyo wafanye utafiti wakujua tatizo hilo lilikuwa na ukubwa gani. “Baada ya kufanya utafiti wao pia walimpata mhusika, ambapo tulischukua jukumu la kwenda kumhoji Mkuu wa washule hiyo ili kujua kama mwalimu Gaudensia alikuwa na akili timamu au la, hata hivyo, Mkuu wa shule atueleza kuwa alikuwa na akili timamu,”alisema Tembo.  Alisem

MWALIMU SHULE WA SEKONDARI KIBASILA AKUTWA AMERUNDIKA KINYESI CHA BINADAMU NDANI KWAKE

Image
Ama kweli dunia ina mambo, na ukistaajabu ya Mussa kweli utayaona ya Firauni kwa mwalimu huyu wa Sekondari ya Kibasila Jijini Dar es salaam ambapo katika hali isiyo ya kawaida Mwalimu Gaudensia Missanga wa shule ya Sekondari Kibasila anayefundisha masomo ya Biolojia na Kemia amekutwa akiishi na lundo la kinyesi cha binadamu chumbani kwake kwa muda mrefu, katika eneo la Temeke Kisiwani. Mwalimu huyu anadaiwa kuishi katika chumba ambacho amehifadhi kinyesi hali ambayo inatishia  usalama wa afya yake. Hebu jenga picha, mwalimu wa shule ya Sekondari halafu anaishi ndani na kinyesi! Hivi hii imekaaje? Tukio hilo la mwalimu huyo kuishi na mrundikano wa uchafu huo liligundulika siku tatu zilizopita eneo la Yombo Kisiwani, Kata ya Sandari wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. Jinsi tukio hili lilivyotokea Mmiliki wa nyumba aliyopanga mwalimu huyo, Ruben Shayo aliliambia gazeti moja hapa nchini kuwa Februari 22 mwaka huu, ulionekana moshi kwenye chumba cha mwalimu

CHID BENZ APONEA CHUPU CHUPU MIAKA MIWILI JELA, ALIPA FAINI YA SH. 900,000

Image
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Rashidi Abdallah Makwaro Maarufu kama (Chid Benzi) amehukumiwa kifungo cha miaka mwili jela au kulipa faini ya shingili laki tisa bada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ikiwemo kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin yenye thamani ya sh. 38,638, bangi ya sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae. Chid Benz alikamatwa mwaka jana katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa na madawa hayo. Mwanamuziki huyo ambaye alikiri kosa hilo wiki iliyopita, alikamatwa uwanjani hapo akiwa anajitayarisha kupanda ndege kwenda Mbeya kwenye tamasha la muziki. Hata  hivyo,  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo   imemwachia  huru mwanamuziki huyo  baada ya kulipa faini ya 900,000/

WALIOMUIBA MTOTO PENDO MWENYE ULEMAVU WA NGOZI WAKAMATWA MWANZA

Image
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, amesema watu wote waliohusika ‘kuiba’ mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (albino) Pendo Emmanuel (4) katika kijiji cha Ndami wilayani Kwimba, Mwanza, wamekamatwa. Akizungumza wakati akiwaapisha wakuu wapya wa wilaya wa mkoa huo jana, Manju Msambya (Misungwi), Zainab Rajab (Sengerema) na Pili Moshi (Kwimba), Mulongo alisema watu wote waliohusika wamekamatwa na hivi sasa bado hawafahamu kama mtoto huyo yupo hai ama mfu.    “Wezi wale baada ya kumuiba mtoto Pendo walimleta katika hoteli moja hapa jijini Mwanza, kisha kuwakabidhi watu walionekana wanunuzi, lakini wote hao wamekamatwa akiwamo mmiliki wa hoteli hiyo,”  alisema Mulongo.    Alisema serikali ipo kazini wakati wote, ndiyo maana inafanya kazi usiku na mchana kuwasaka watu wote waovu mkoani Mwanza ambao hawawezi kusalimika kwa kile watakachokifanya.    Hata hivyo, alisema watu hao waliofanya uhalifu huo akiwamo baba wa mtoto huyo, Emmanuel Shilinde, wanashikiliwa na polisi huku mtu wa mw

CHENGE AGOMA KUHOJIWA NA SECRETARIETI YA MAADILI YA UMMA

Image
Adai kuna zuio la mahakama kuu Hatma yake yajulikana leo MBUNGE wa Bariadi Magharibi, Mtemi Andrew Chenge, jana ameonyesha utemi wake mbele ya Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma, baada ya kusema haiwezi kumjadili kwa sababu kuna kesi mahakamani.   Alisema kuna zuio la Mahakama Kuu ambalo limevitaka vyombo vyote vya Serikali kutojadili suala la miamala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hadi kesi ya msingi itakapoamuliwa.   Tume hiyo inamtuhumu mbunge huyo kuwa alipokuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, alitumia madaraka yake vibaya katika uuzaji wa hisa za Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kwenda Kampuni ya VIP Engineering Tanzania Limited.   Itakumbukwa wakati suala la Tegeta Escrow likijadiliwa bungeni, Chenge alidaiwa kupewa sh bilioni 16 na mmiliki wa VIP Engineering Tanzania Limited, James Rugemalira.   Jana, kabla ya Chenge kuieleza Tume ya Maadili kuwa haiwezi kumuhoji, Mwanasheria wa tume hiyo, Hassan Mayunga, alisoma mashtaka yanayomkabil

VURUGU ILULA MKOANI IRINGA POLISI WAUWA, WANANCHI WACHOMA MOTO KITUO CHA POLISI

Image
Inasemekana polisi walivamia eneo la kilabuni na kuanza kupiga kila raia na kusababisa kifo cha huyo mama muuza Pombe za kienyeji. Kosa ni kufungua kilabu cha Pombe kabla ya muda ulioruhusiwa kisheria. Wananchi wamechoma matairi barabara Kuu hakuna gari inayopita, Polisi bado hawajafika waliopo wamekimbia baada ya kuzidiwa na wananchi. Baadae gari tatu zilizosheheni FFU zimewasili mabomu yanapigwa mfululizo, sasa hivi wanasafisha barabara kwa kuzima moto na kutoa matairi njiani. WANANCHI wenye hasira mjini Ilula, mkoani Iringa, wamevamia kituo cha polisi na kuvunja milango kisha kuwafungulia mahabusu waliokuwemo ndani, wakachoma moto baadhi ya magari yaliyokuwepo kituoni hapo pamoja na mafaili. Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, tukio hilo limetokea leo asubuhi kufuatia mwanamke ambaye hakufahamika jina lake kujigonga ukutani na kuanguka kisha kufariki dunia wakati akiwakimbia polisi waliokuwa kwenye oparesheni ya kuwakamata watu wanaokunywa pombe wakati wa asubuhi. Habari zaidi

STOP KILLING ALBINO TANZANIA, LET'S SAVE LIFE

Image
Think about the generations and say we wanna make it a better place For our children and our children's children So that they know what's a better world for them And think they can make it a better place There's A Place In Your Heart And I Know That It Is Love And This Place Could Be Much Brighter Than Tomorrow And If You Really Try You'll Find There's No Need To Cry In This Place You'll Feel There's No Hurt Or Sorrow There Are Ways To Get There If You Care Enough For The Living Make A Little Space Make A Better Place... Heal The World Make It A Better Place For You And For Me And The Entire Human Race There Are People Dying If You Care Enough For The Living Make A Better Place For You And For Me If You Want To Know Why There's A Love That Cannot Lie Love Is Strong It Only Cares For Joyful Giving If We Try We Shall See In This Bliss We Cannot Feel Fear Or Dread We Stop