MBAGALA ILIVYOKUWA LEO,MABOMU YA MACHOZI YATAWALA





Jeshi la Polisi Mkoani Dar es Salaam limetumia nguvu kwa  kurusha mabomu ya machozi ili kuwatawanya wanachama  wa  chama  cha Wananchi CUF waliokuwa kwenye maandamo wilaya ya Temeke  nakufanikiwa kuwatia nguvuni viongozi waandamizi wa chama cha Wananchi CUF,wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Profesa Ibrahimu Lipumba.
Akithibitisha kukamatwa viongozi hao pamoja na kuvunjwa kwa maandamano, Afisa habari wa chama cha Cuf ,Bwana Silas  alipoongea na mtandao huu amesema waalianza maandamano ya Amani katika Viwanja vya temeke na kwenda mbagala , ambapo maandamano hayo yalikuwa na lengo la kumbukumbu ya mauaji ya wanachama wao yaliofanyika  Tarehe 26 januari mwaka  2001 huko Zanzibari na Tanzania Bara.
 
Bwana Silas alisema wakati wapo kwenye maandamo hayo walipofika maeneo ya Mtongani iliyopo wilaya ya Temeke ndipo Jeshi la polisi likafika na kurusha mabomu na kuwapiga wanachama wa chama hicho na kufanikiwa kuwakamata viongozi wa chama hicho na kuwapeleka kituo kikuu cha polisi kwa madai kuwa  maandamano hayo hayakuwa na ruhusa.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI