MAMA AMFUKUZA MWANAE NA KUMTAKA AKAPANGE CHUMBA KISA KAUNGUZA MBOGA



Mtoto wa miaka 12 mkazi wa Mkoa wa Geita ametimuliwa nyumbani na mama yake mzazi na kutakiwa kwenda kuishi maisha ya kujitegemea baada ya kuunguza mboga jikoni.

Mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya Msingi Karangalala ameamuriwa na mama yake kufanya hivyo baada ya mama yake Helena kumwachia jukumu la kupika mboga Novemba mwaka jana lakini mboga hiyo iliungua.

Baada ya kuunguza mboga hiyo,mama huyo alimpiga mwanaye kabla ya kumpa masurufia na kumkabidhi chumba tayari kwa kuanza maisha.

Mtoto huyo alisema mama yake amekua na tabia ya kumpiga mara kwa mara kiasi cha kusababisha mwili wake kuwa na alama za viboko.


“Sifahamu kwa nini mama yangu huwa ananipiga kiasi hiki,inawezekana kwa kuwa na yeye alilelewa na mama wa kambo aliyekua anampiga hivi”alisema mtoto huyo.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI