AMTOBOA BINTI YAKE MACHO NA YEYE KUJINYONGA


                 Agripina Godfrey


                      Godfrey Joseph Kajuna akiwa amejinyonga


Mkazi mmoja aishiye katika Kitongoji cha Buyumba,Kijiji cha Bushemba,Kata ya Buganguzi Wilayani Muleba Mkoa wa Kagera anayefahamika kwa majina ya Godfrey Joseph Kajuna (45miaka) amejinyonga hadi kufa (Kama picha zinavyoonesha.

Sababu iliyopelekea kifo cha Baba huyo ni baada ya huyo Baba kumpiga mtoto wake wa kumzaa. Inasemekana kuwa alimpiga na kumjeruhi kichwani kwa fimbo nzito kisha akamtoboa macho, mtoto huyo anafahamika kwa jina la Agripina Godfrey (12) anayesoma Darasa la Kwanza ktk S/M Ilambika.

Sasa kisa kizima ni kwamba Baba alitoka ndani na kuwambia wanae kuwa Mama yao akirudi wasimfungulie mlango…
Hivyo mama aliporudi watoto kwa kumuogopa Baba yao wakakataa kata kata kumfungulia Mlango.
Basi Mama akaondoka kujiweka sehemu.

Baba yao aliporudi akawauliza Mama yao yuko wapi,ndipo huyo mtoto aliyeonekana kama ndo mkubwa kwenye familia hiyo akamjibu Baba yake kuwa "Baba si ulisema mama akija tusimfungulie?" Hali hiyo ikamfanya Baba yake aanze kumpiga saana! Mpaka kumuumiza vile.

Sasa damu zikaanza kumtoka mtoto,Baba mtoto akachukua Chumvi na kuanza kuimimina kwenye jeraha kichwani(hiyo nyeupe kwenye Picha)

Basi mtoto alipoonekana kama hali inakuwa Mbaya… Baba akaandika kijibarua haraka na kusema kuwa kwa kitendo alichofanya na vitendo vingine ambavyo huwa anaifanyia familia hiyo ameogopa kukamatwa… akajitundika kwenye Kamba na kujimaliza yeye mwenyewe. Mtoto alipelekwa katika Hospitali teule ya Wilaya ya Muleba (Rubya Hospital) kwa matibabu zaidi.

Maelezo haya na Picha yametolewa na Afisa Mtendaji Kata ya Buganguzi Bwana Wilson Dickson.




Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI