DAMU,AGANO NA SADAKA


Agano ninini?
Agano ni mapatano  au makubaliano kati ya mtu na mtu, mtu na Mungu au mtu na mizimu.
Agano la Mtu na mizimu
Agano hili hufanyika kwa njia ya damu na sadaka, Mtu anapoenda kwa mganga wa kienyeji na kuchanjwa chale tayari ameshafanya agano kwenye madhabahu ya mganga wa kienyeji ambaye ni wakala wa shetani. Hivyo anapotoa ile damu tayari umeshajiunganisha na madhabahu ile wewe ni mtumwa wa kuzimu hivyo huwezi kufanya jambo lolote bila idhini/ruhusa ya hao ‘’waliokununua‘’ kwa damu yako mwenyewe .

(KUTOKA 34:12)
Ujihadhari nafsi yako usije ukafanya maagano na wenyeji wa nchi ile unayoiendea usije ukawa mtego katikati yako.13Bali utabomoa madhabahu zao na kuvunja vunja kazi zao  na kuyakata maashera yao.15Usije ukafanya agano na wenyeji wan chi watu wakaenda kufanya uzunzi na miungu yao na kuitolea sadaka miungu yao mtu mmoja atakuita ukila sadaka yake.

(WALAWI 17:11)
Kwakuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu,name nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu ili kufanya upatanisho juu ya nafsi zenu kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi .
Kwahiyo Kuokoka ni jambo moja,  na kuvunja agano ni jambo lingine usije ukajifariji kuwa ukioka umekuwa kiumbe kipya ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya .Hivyo hata kama umeoka huwezi kufanikiwa usipovunja agano na madhabahu uliyomwaga damu yako

AGANO LA SADAKA KATIKA MADHABAHU ZA KUZIMU  LINAVYOWEZA KUKUZUIA KUFANIKIWA

Watu wengi  wanafanya kazi kwa bidii na kupata pesa nyingi lakini mwishoni pesa zao kuisha bila wao kujua hii inatokana na zile hela ulizokuwa unatoa kule kwa mganga wa kienyeji kama nilivyosema awali kuwa ukisha fanya agano nao lazima watakufanya mtu wao chochote utakachofanya ni kwa ajili yao hata pesa ukitafuta ni zao maana wewe ni mtumwa wao

JINSI YA KUJIKOMBOA NA KUJITOA KWENYE MADHABAHU HIZO

Kama ambavyo ulifanya agano kwenye madhabahu hizo kwa njia ya damu na sadaka na wewe hiyo hiyo unatakiwa ujitoe huko kwa njia ya damu na sadaka vile vile.

(WALAWI 16:6)
Na Haruni atatoa Yule Ng’ombe wa Sadaka kwa ajili ya dhambi zake, aliye kwa ajili ya nafsi yake  na kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake yeye mwenyewe na Nyumba yake.

By Evangelist Prisca E Mwang'ombola 

SOMO LINALOFUATA

JINSI MTU ANAVYOWEZA KUPATA LAANA NA MIKOSI KWA  NJIA YA KUJAMIIANA/KUZINI.



Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA