YANGA SC YAPIGWA 2-0 JAJA AKOSA PENALTI MOROGORO

                                               Kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar
                     Mashabiki wa timu ya Yanga SC wakishangia wakati wa mchezo

                                     
                      Kipa wa Mtibwa Sugar Saidi Mohames akiokoa  Shambuluzi la Yanga CS

                                        
                                                                        Yanga SC

         Yanga SC imeanza kwa kipigo cha mabao mawili Ligi kuu ya Vodacom Tanzania  Bara kutoka kwa Mtibwa Sugar uwanja wa Jamhuri Morogoro mshambuliaji Genilson Santana 'Jaja' akikosa Penalti
        Katika mchezo huo uliyochezeshwa na refa  Dominic Nyamisana wa Dodoma aliyesaidiwa na Ferdinand Chacha wa Mwanza na Milambo Tshikungu wa Mbeya. Hadi mapumziko tayari Mtibwa Sugar wanaongoza kwa kwa bao 1-0.
        Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji wa zamani wa timu ya Simba SC Mussa Hassan Mgosi katika dakika ya 16,Aliyemalizia pasi ya kichwa ni Ame Ali na na kumuwahi kipa Deo Munishi aliyetokea vizuri katika kudaka. Mfungaji wa bao la pili la Mtibwa Sugar ni Ame Ali dakika ya 82 kipindi cha pili.
       Yanga SC; Deo Munishi,'Dida' Juma Abdul, Oscar Joshua,Omega Seme, Nadir Haroub 'Cannavaro' Kevin Yondan, Mbuyu Twite , Said Bahanuzi,Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima, Gelson Santana 'Jaja', Mrisho Ngassa na Hamisi Kiiza /Simon Msuva.


      



























































Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA