WACHUNGAJI MBARONI KWA KULAWITI WATOTO KANISANI


 Watoto sita waliobakwa kanisani na watu wanaodaiwa ni wachungaji

         Watoto sita wakiwemo wawili wa kiume wenye umri wa miaka 8 hadi 14 wamwharibiwa vibaya sehemu zao za siri baada ya kubakwa kanisani na watu wanaodaiwa kuwa ni wachungaji.
        Wakiwa katika Hospital ya Mountmeru, Arusha walikipelekwa kwa matibabu na kuangaliwa maambukizi ya magonjwa ya Zinaa, watoto hao walidai kufanyiwa mchezo huo kwa nyakati tofauti na wachungaji watatu wa kanisa hilo lililopo eneo la Feed Force, Kwamorombo jijini Arusha. Mmoja wa watoto hao anayesoma darasa la nne aliyeleza kuwa yeye na wenzake walikuwa wakifanyiwa mchezo huo mchafu na wachungaji hao baada ya kuwapatia sh. 2000 za kufunga mdomo.
      ''Siku moja nilipofika shuleni wenzangu wakaniambia niende kanisani hapo nikapewe hela nilipofika niliwaona wenzangu wakifanyiwa mchezo mchafu na mimi mchungaji aliniambia niiname akanifanyia mchezo huo mchafu na kunipa sh 2000 niliumia sana'' alisema mwanafunzi mmoja.
      Mwanafunzi mwingine alisema alikuwa anatoroka shuleni na wenzake na kwenda kwa watumishi ambapo huwaingiza katika kanisa hilo na kujifanya wanawaombea na baadae kuwafanyia mchezo mbaya       ''Tukifika wanatufungia ndani na kutuambia tuwanyonye ,baadaye wanatuambia tukusema tu wanatubaka na kutuambia tukisema kwa mtu yoyote watatuchinja na kutuzika ndani ya kanisa lao'' alisema mwanafunzi huyo
      Wanafunzi hao walisema watumishi hao wa Mungu huwarubuni kuwa watawasaidia watawasomesha iwampo watakuwa anaenda kwenye kanisa hilo na kuwaingilia. Mzazi mmoja wa watoto hao Julius , mkazi wa Kwamorombo alisema mtoto wake alikuwa akifanyiwa mchezo mbaya baada ya kupatiwa sh 2000.Alisema amegundua hilo baada ya mtoto wake kuchelewa kurudi Nyumbani.
       Watoto baadae walihamishiwa katika Hospitali ya Seriani kwa ajili ya vipimo huku taarifa za awali na madaktari wa Hospitali hiyo kuwa Baadhi yao walikuwa na michubuko na kupanuka sehemu za siri hali inayoonyesha kuingiliwa.Watuhumiwa hao wameshikiliwa katika kituo kikuu cha polisi Arusha kwa uchunguzi zaidi na Kamanda wa Polisi Arusha Rebelatus Sabas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.




























Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA