VURUGU SHOW YA DIAMOND SIRI ZAFICHUKA



      




           Siku kadhaa baada ya promota mwenye asili ya Nigeriakukamatwa kufuatia sakata la vurugu ya Msanii Diamond, siri kadhaa zimeibuka kufutia kisa hicho kilichomsibu msanii huyo mjini Stuttgart,Ujerumani.

SIRI YA KWANZA ; KIBALI
          Imebainika kuwa , katika sakata hilo lililojiri wiki mbili zilizopita, Promota huyo aliwadanganya wamiliki wa ukumbi wa Sindelfingen uliopo mji wa Stuttgart, Ujerumani kuwa kutakuwa na mkutano wa Waafrika waishio nchini humona baada ya hapo kutakuwa na Part ya kawaida.
     

SIRI YA PILI; UTEKAJI

         Nikwamba Diamond alikuwa atekwe kwani kulikuwa na waandaaji watatu wa mpango huo, hivyo wawili walipanga wamteke akafanye kazi sehemu nyingine.

SIRI YA TATU; BIMA

       Ukiachana na uongo wa Promota Awin, imebainika kuwa hakukuwa na bima ya kulinda usalama wa watu endapo litatokea tatizo km ambavyo lilitokea na watu wengi kujeruhiwa.

SIRI YA NNE; UKUMBI WA MIKUTANO

       Kingine ni kwamba hata hivyo ukumbi ulibainika kuwa sio wa kufanyia show za miziki bali ni kwaajili ya maonyesho ya bidhaa.

SIRI YA TANO; HASARA MIL. 600

          Baada ya uchunguzi kufanyika imebainika kuwa hasara iliyosababishwa na vurugu hizo ni Euro 300,000 ambazo ni zaidi ya milioni 600 za Kitanzania Hivyo Awini anatakiwa awalipe wamiliki wa ukumbi huo

  SIRI YA SITA; KESI

      Licha ya Promota huyo kufikishwa polisi kwenye mji wa Stuttigurtsuala lake lipo chini ya ofisi ya mji huo ili sheria ichukue mkondo wake huku polisi wakisisitiza kwamba Diamond akitia mguu tu watamdaka.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA