MAANDAMANO YALIYOPANGWA NA CHADEMA YAZUIWA NA POLISI DODOMA

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi Emmanuel G. Lukula.

      Jeshi la polisi limetoa tamko la kuia maandamano yaliyopangwa na CHADEMA ya tarehe 18/09/2014 na kuwataka wananchi kuyapuuza.  Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi wa Polisi Emmanuel G Lukula , alisema kuwa; Kufuatia viongozi wa CHADEMA kutaka kufanya maandamano kuelekea ofisi za Bunge Dodoma kwa ajili ya kupinga Bunge la katiba alisema kuwa maandamano hayo ni batili. Kamanda Likula alitaja sababu za kuzuia maandamano hayo ni ;
  1.  Siku ya  maandamano tarehe 18/09/2014 ni siku ya kazi ikiwa pamoja na muda wa maandamano hayo kuwa ni masaa ya kazi saa 4:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana yataathiri ufanisi wa watu walioko kazini.
  2. Bunge la katiba linaloendelea sasa lipo kisheria na hakuna tamko lolote lililotolewa na mahakama yoyote kulisitisha hivyo moja ya kazi za Polisi ni kulinda sheria na wale wanaofuata Sheria.
  3. Kuna kesi Mahakamani kupinga Bunge hilo kuendelea, hadi sasa shauri hilo linaendelea Mahakamani hivyo kwa CHADEMA kuandamana ni kuingilia Uhuru wa Mahakama.
  4. Baadhi ya Barua za kufanya maandamano zimechelewa kwa wakuu wa Polisi Wilaya kabla ya saa 24 Kisheria.
        Aidha aliwashauri viongozi wa CHADEMA Mkoa na Wilaya za Dodoma wasitishe maandamano hayo wasiporidhika wakate Rufaa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwa maelekezo zaidi.




Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA