MWALIMU AKUTWA AMEFUNGWA MINYORORO KANISANI





           Ndugu wa mtu anayedaiwa kuwa ni ulemavu wa akili Galus Focus Nguruwe ambaye ni mwalimu wa Sekondari moja mjini Morogoro, wamelituhumu kanisa la House of Prayer Shieid of Faith Christian Fellowship lililopo Boko magengeni Jijini Dar kuwa wamemfunga ndugu yao huyo kwa miezi nane mfululizo.

        Kwa mujibu wa dada wa Galusi Piencia Focus, ndugu yao huyo alichukuliwa na mtoto wa dada yao  aliyetajwa kwa jina la Doreen anayeishi Songea Mkoani Ruvuma Januari mwaka huu bila kuwataarifu ndugu jambo lililowafanya wafuatilie na kugundua kuwa amepelekwa kwenye kanisa hilo kwa madai ya kuwa amepelekwa kufanyiwa maombi.
        Ndugu wamesema waliamua kumtafuta ndugu yao huyo baada ya kupata taarifa kuwa ndugu yao anaishi huku amefungwa minyororo mguuni hali inayomfanya ajisaidie na kula hapo hapo
Japo kuwa alikuwa na matatizo ya akuli lakini alikuwa akitumia Dawazake na kupata nafuu na kufanya kazi yake ya ualimu kwani alikuwa akifundisha shule moja iliyopo Morogoro.
Ndungu hao walifika kituo cha polisi Wazo Hill na kufungua jalada lenye namba za kumbukumbu WH/RB/6364/14 WIZI TOKA MAUNGONI.

Mwalimu Galus Focus Nguruwe akiwa amefungwa mnyororo

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA