JAJA ASHAURIWA KUONDOKA NCHINI

        Klabu ya mtibwa Sugar imesema kuwa Straika wa Yanga Mbrazili Geilson Santos 'Jaja' atachemka katika ligi ya Bongo na kusisitiza ingekuwa busara kama wangemuandalia mapema nyaraka zake ili arejee kwao kuendelea na majukumu mengine.
        Kitendo cha Yanga kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Mtibwa juzi jumamosi kwenye uwanja wa jamhuri, Morogoro kimeendeleza 'uteja' wa timu hiyo katika uwanja huo kwani kwa mara ya mwisho Yanga kuibuka na ushindi katika timu hiyo ilikuwa ni Septemba 19,2009.ikiwa chini ya kocha Dusan Kondic.
       ''Tumeanza kuibabua Yanga na Jaja wao maana kila mara ilikuwa ni Jaja, Jaja Jaja huyo Jaja ndio nani? amefichwa na mabeki imara hakuonekana kabisa uwanjani''walisema.
       Waliongeza kuwa Jaja ni ni Straika mwenye umbo zuri,na siyo uwezo uwanjani unajua timu zetu hizi zinaamini watu kutoka nje kuliko vijana wa hapa kitu ambacho si sahihi.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA