MECHI YA SIMBA,YANGA OCTOBA 12 YAAHIRISHWA.

          Ile mechi ya Yanga dhidi ya Simba imesogezwa mbele na TFF haijasema itakuwa siku gani.Badala yake siku hiyo kutakuwa na mechi ya Taifa Stars.Timu ya Taifa, Taifa Stars itashuka uwanjani octoba 12 mwaka huu kuikabili Benin katika Mechi ya kirafiki ya kalenda shirikisho la Kimataifa la mpira wa Miguu FIFA
      Mechi hiyo itachezwa uwanja wa Taifa Dar es salaamkuanzia saa kumi kamili jioni.Program ya Taifa Stars inayodhaminiwa na na Kilimanjaro premium Lager kwa ajili ya mechi hiyo itatangazwa na na kocha mkuu Mart Nooij.
      Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania linaendelea na taratibu nyingine kwa ajili ya mechi hiyo ikiwemo usafiri wa Benin kuja nchini ambapo timu hiyo inatarajiwa kutua Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Oktoba 10 mwa huu ikiwa na msafara wa watu 28.
      Pambano la Stars na Benin litatanguliwa na mechi ya kudumisha upendo kati ya viongozi wa dini ya Kiislam na Kikristo.
      Wakati huo huo  kutokana na mechi hiyo ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom inafanyiwa marekebisho madogo na marekebisho hayo yatatangazwa kesho Septemba 26.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA