SERENGETI FIESTA SHINYANGA



           Tamasha la Serengeti Fiesta 2014  limefanyika leo limefanyika usiku wa kuamkia leo katika uwanja
 mdogo  wa Kambarage ambapo kila msanii aliyepanda alipata shangwe za kutosha.

            Msanii wa kwanza kupanda jukwaani alikuwa ni Mo Music,Baadae alishuka na kumkabidhi kipaza sauti mwana dada Khadija, Mwana dada Khadija alisumbua na wimbo wake wa Maumivu, ambaye alimuachia Rachel na kumpisha Young Killer .
                                                                              
              Makamuzi yaliendelea yalizidi kushika kasi baada ya Ommy Dimpoz kupanda jukwaani na kumpa pasi Stamina ambaye aliamua kumuachia Nay wa Mitego  aliyempisha mtangangazaji wa Clouds Fm AdamMchomvu ambaye alimpandisha Mwana dada Linah.
   
           Shangwe zilikolea zaidi baada ya Mr. Blue kupanda jukwaani na baadae kuwapisha Chegge na Temba walifanya show kali na kumpisha Nickki wa II ambaye alifanya yake na kumpa kipaza Fid Q ambaye alifunga pazia la burudani.

                                                                            

                                                  
Nay wa Mitego katika Jukwaa
Msanii Rachel akitumbuiza                                    
                                                   Linnah akiwa na madansa wake

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA