PHIRI AMTULIZA TAMBWE SIMBA SC

   












                                                  AMISSI TAMBWE

          Baada ya kumuacha  katika kikosi cha timu hiyo kilichocheza dhidi ya URA ya Uganda hivi karibuni. Kocha Mkuu wa Simba , Patrick Phiri  amemtuliza mshambuliaji wake raia wa Raia wa Burundi  Amissi Tambwe na kumhakikishia kuwa atapata nafasi ya kucheza.

       Ijumaa iliyopita mchwzaji huyo alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kutoswa katika kikosi hicho ambacho kilicheza na URA na kulazimishwa kutangulia kwa Basi mkoani Mtwara akiwa na wachezaji wengi wa timu B kwa ajili ya mechi ya juzi jumamosi ya kirafikidhidi ya Ndanda FC kwenye uwanja wa NangwandaSijaona.Hali hiyo ilimsikitisha Tambwe na kuona maisha yake kilabuni hapo kuwa machungu kama shubiri huku furaha aliyokuwa nayo msimu uliyopita ikitoweka.

       Kocha Phiri alimuita na kuzungumza nae na kumhakikishia kuwa atapata match ya kucheza katika kikosi chake cha kwanza hivyo anatakiwa kutulia.
Tambwe kwa sasa hana uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza kutokana na washambuliaji Emmanuel Okwi na Paul Kiongera kuwa chaguo la kwanza la Phiri.
 .

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA