MLIPUKO WAUWA 12 NCHINI CHINA

         Taswira kutoka eneo la Kiwanda cha Nanyang ulipotokea mlipuko

        Takribani watu 12 wamwfariki katika mlipuko huku 33 wakiwa wamejeruhiwa katika mlipuko uliotokea jana katika kiwanda cha kutengenezea Fataki jijini Liling katika Mkoa wa Hunan Nchini China
      Moto huo ulitokea katika kiwanda cha Nanang ambapo wahusika hawakutaja chanzo chake. Matukio ya milipuko katika viwanda vya fataki Nchini China yanazidi kuongezeka ambapo mwaka jana mlipuko mwingine ulitokea katika kiwanda kilichopo Guangxi na kuua watu 11 huku 17 walijeruhiwa.
     Februari mwaka jana gari lililokuwa limebeba mafataki nalo lililipuka barabarani katika mkoa wa Henan na kuua watu wa tano na kuharibu sehemu ya barabara.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA