DAMU,AGANO NA SADAKA
Agano ninini? Agano ni mapatano au makubaliano kati ya mtu na mtu, mtu na Mungu au mtu na mizimu. Agano la Mtu na mizimu Agano hili hufanyika kwa njia ya damu na sadaka, Mtu anapoenda kwa mganga wa kienyeji na kuchanjwa chale tayari ameshafanya agano kwenye madhabahu ya mganga wa kienyeji ambaye ni wakala wa shetani. Hivyo anapotoa ile damu tayari umeshajiunganisha na madhabahu ile wewe ni mtumwa wa kuzimu hivyo huwezi kufanya jambo lolote bila idhini/ruhusa ya hao ‘’waliokununua‘’ kwa damu yako mwenyewe . (KUTOKA 34:12) Ujihadhari nafsi yako usije ukafanya maagano na wenyeji wa nchi ile unayoiendea usije ukawa mtego katikati yako. 13 Bali utabomoa madhabahu zao na kuvunja vunja kazi zao na kuyakata maashera yao. 15 Usije ukafanya agano na wenyeji wan chi watu wakaenda kufanya uzunzi na miungu yao na kuitolea sadaka miungu yao mtu mmoja atakuita ukila sadaka yake. (WALAWI 17:11) Kwakuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu,name nimewapa ninyi hiyo damu juu...