WEMA KUACHANA NA DIAMOND: MAMA WEMA ASHEREHEKEA


Wema Sepetu ‘madam’ akifurahi na mama yake, Mariam Sepetu

Supastaa ‘grade one’ wa sinema za Bongo, Wema Sepetu ‘madam’ akipozi.



          Wema Sepetu,'Madam' akiwa na Diamond Platinumz.



CHEREKO chereko! Siku chache baada ya supastaa ‘grade one’ wa sinema za Bongo, Wema Sepetu ‘madam’ kummwaga King of Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, mama mzazi wa mwigizaji huyo, Mariam Sepetu ameangusha sherehe ya nguvu kama ishara ya kuonesha ‘amekunwa’ na tukio hilo,

kutokana na mama huyo kutobariki uchumba wa mwanaye na Diamond ambaye pia anajulikana kwa jina la Dangote kwa muda mrefu, habari za uchumba huo kuvunjika zilipochapishwa kwenye Gazeti la Ijumaa ‘Kubwa’ toleo lililopita, moyo wake ulijawa na furaha.
“Mama Wema alichukizwa kwa kiasi kikubwa na mapenzi ya wawili hao kutokana na kile alichoamini kuwa, Diamond hakuwa na mapenzi ya dhati kwa mwanaye zaidi ya kutegemea nyota yake impe mafanikio ndiyo maana akafanya pati hiyo fupi nyumbani kwake Sinza-Mori, Dar,” kilisema chanzo hicho.

 Mama Wema alipiga cherekochereko za kutosha siku hiyo kwani alikuwa akimchukia Diamond kwa  muda mrefu.
“Mama Wema chuki zake kwa Diamond hazitaisha kamwe kwa kuwa hampendi tu kutokana na kuona mwanaye hasongi mbele kimaendeleo kama alivyo Diamond ambaye akiachana na Wema mambo yake hayamwendei vizuri kama anavyokuwa na mwanaye.”“Mimi naona huu ndiyo mwisho wa Wema na Diamond na siku zote nasema hakuna uhusiano ukadumu bila baraka za wazazi, niseme tu, sitaki kumuona ndugu yeyote wa Diamond kwangu, kama mahari wakatoe kwa Penny siyo kwa mwanangu,” alisema mama Wema.
TUJIKUMBUSHE
Kumwagana kwa Wema na Diamond safari hii, ni mara ya nne. Awali walimwagana, wakarudiana, wakamwagana tena, Diamond akatua kwa Jokate Mwegelo, wakarudiana tena na Wema, wakaja mwagana tena, Diamond akatambaa na Penniel Mungilwa ‘Penny’, wakamwagana, karudiana na Wema, sasa  wamemwagana tena.


Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA