HOJA ZA WARIOBA MWIBA KWA CCM


Hoja zawaumiza CCM, Makonda aongoza vijana kumshambulia
Mdahalo wavunjika, polisi waonyesha udhaifu
Meseji za kupanga vurugu zanaswa, wanavyuo wahusishwa






Baadhi ya vijana walioandaliwa wakiwa wamebeba mabango yasemayo "Katiba iliyopendekezwa tumeipokea tunaunga mkono"






Jaji Warioba akitoa Mada






HOJA mbalimbali za aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, jana ziliwafanya baadhi ya makada wa CCM kupandwa na jazba na kuzua vurugu kubwa katika mdahalo ulioitishwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere kujadili masuala yaliyomo katika Katiba iliyopendekezwa.

Mdahalo huo ambao ulipangwa kuhutubiwa na baadhi ya wajumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ilibidi uvunjike kutokana na vurugu hizo kubwa.

Mbali na kuvunjika kwa mdahalo huo, pia Jaji Warioba ambaye pia ni Makamu wa Rais mstaafu katika serikali ya awamu ya Pili, alishambuliwa kwa kupigwa na Katibu wa Uhamasishaji wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, pamoja na wafuasi wengine wa chama hicho.

Kabla ya kuanza kwa vurugu hizo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, aliwaeleza wananchi waliohudhuria mdahalo huo dhamira yake ni kupata ufahamu wa masuala yaliyomo katika katiba na yale yaliyoondolewa, pia kufikia uamuzi sahihi siku ya kupiga kura ya kukataa au kukubali katiba hiyo.

Mara baada ya Butiku kumaliza kuongea, alimkaribisha mtoa mada Jaji Warioba, ambaye alizungumzia masuala mbalimbali yaliyoboreshwa na kuondolewa.

Muda wote Warioba alipokuwa akizungumza, wananchi walikuwa wakimshangilia kwa makofi huku baadhi ya vijana waliopangwa kufanya vurugu wakiwa wanahimizana kuonyesha mabango yao waliyoyaandaa juu.

Vurugu zilivyoanza

Vurugu mdahalo wavunjikaWakati Jaji Warioba akizungumzia masuala mbalimbali, alilalamikia kitendo cha watu kumtumia Mwalimu Nyerere kama kinga ya kufanikisha masuala yao, huku akieleza kuwa kiongozi huyo mpaka anafariki dunia alikuwa akiamini katika azimio la Arusha.“Laiti kama Nyerere angekuwepo asingekubali viongozi kuweka fedha nje ya nchi, kama Nyerere angekuwepo asingekubali viongozi kupewa zawadi na kuzificha majumbani mwao na kama Mwalimu Nyerere angekuwepo katika zama hizi…asingeruhusu maadili ya viongozi kukataliwa kuingizwa katika katiba,” alisema Jaji Warioba.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA