MALIPO YA KASEJA YAZUA UTATA YANGA

                                                    Juma Kaseja 
YANGA wameibuka na hoja ya kwamba tayari wameshamalizana na madai ya fedha za kipa wake Juma Kaseja lakini meneja wa kipa huyo ameshtushwa na taarifa hizo akisema hakuna lolote, huo  ni ubabaishaji.
Katibu wa Yanga, Benno Njovu, alisema tayari uongozi wake ulishamalizana na Kaseja juu ya kiasi cha fedha alichokuwa anadai. Meneja wa Kaseja, Abdulfatah Saleh alisema: “Nimesoma katika vyombo vya habari katibu wao akisema hanitambui mimi, lakini mimi pia naweza kusema hata yeye simtambui kwa kuwa wakati Yanga wanamsajili nilifanya mazungumzo na mabosi wake wa juu Isaac Chanji, Abdallah Bin Kleb na Seif Ahmeid waliokuja ofisini kwangu.
“Wakumbuke kwamba Kaseja alikataa kabisa kupokea fedha nusu lakini nilimsihi apokee ili niweze kuwasaidia viongozi wenzangu ambao nawaheshimu sana, akakukabali kulipwa nusu sasa kama wao wanasema wamelipa wataje wamelipaje hizo fedha na kazipokea nani hakuna sababu ya malumbano.”

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI