APIGWA RISASI NA KUFARIKI DUNIA LEO ASUBUHI


Mwili wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Betty baada ya kupigwa risasi asubuhi ya leo, Yombo Vituka, Temeke  jijini Dar es Salaam akiwa kwenye gari aina ya Toyota Pick Up ya Tunu Security na watu waliokuwa na bodaboda.…




                     Wananchi wakiwa eneo la tukio.





Mwili wa marehemu Betty ukibebwa na polisi kupelekwa hospitali ya Chang'ombe kwa uchunguzi.


Mtu asiyefahamika (mwenye simu katikati) akiwasiliana na ndugu wa marehemu betty baada ya kufika eneo la tukio.



Dada aliyefahamika kwa jina la Betty amepigwa risasi leo saa mbili asubuhi maeneo ya Lumo - Yombo Vituka, Temeke jijini Dar es Salaam akiwa kwenye gari aina ya Toyota Pick Up ya Tunu Security walikuwa wanatokea kituo cha mafuta wanaelekea benki mjini.

Watu waliokuwa kwebnye Bodaboda mmoja alimpiga dereva wa gari hiyo risasi ya mkononi halafu akampiga Betty risasi ya kichwani  na mlinzi aliyekuwa katika gari hiyo alikimbia na watu hao kuchukua mfuko uliokuwa na pesa na kutokomea kusikojulikana na baadae mwili wa marehemu kuchukuliwa na polisi na kupelekwa hospitali ya Chang'ombe kwa ajili ya uchunguzi.




Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA