LUNDENGA AFUNGUKA KUHUSU SITTI MTEMVU



Mkurugenzi wa Lino Agency Hashim Lundenga

Mkurugenzi wa Lino Agency ambao ni waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga amefunguka na kuweka wazi kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na aliyekuwa mshindi wa kwanza wa Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu.Lundenga amefunguka hayo jana alipokuwa akichata Live kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live kinachofanyika kila siku ya Jumatano kuanzia saa sita mchana mpka saa nane mchana. Mbali na mahusiano Watu wengi walitaka kujua ni sifa zipi zilizompelekea mrembo Sitti Mtevu kutwaa taji hilo kama si upendeleo kutoka katika kamati na crew inayohusika kuandaa mashindano hayo kwani watu wengi wamekuwa wakisema kuwa mrembo huyo alikuwa hastahili kushinda taji hilo ukilinganisha na warembo wengine ambao walikuwa wakichuana nae,kufuatia hali Ludenga ikabidi aweke wazi sifa tano amabzo zinamfanya mtu kushinda taji la Miss Tanzania kuwa ni lazima awe na sura nzuri, umbo zuri, mvuto, haiba, ufahamu wa kutosha wa mambo mbali mbali. SITI HANA SIFA YA KUWA MISS TEMEKE Kutokana na maamuzi ambayo Sitti Mtevu aliamua kujivua taji la Miss Tanzania 2014 hivyo mrembo huyo amejifutia sifa zake zote alizopata katika kusaka taji la Miss Tanzania hivyo si Miss Chang'ombe wala si Miss Temeke tena. Hashim Lundenga amesema kuwa kitendo cha Sitti kujivua taji hivyo automaticaly amevua mataji yake yote aliyopata katika ngazi ya wilaya mkoa na hata Taifa kama ambavyo ilivyotangazwa. "Hashim Lundenga: Automatimacally anakuwa amejivua na mataji mengine pia...." Kufuatia sakata la Mrembo Sitti Mtevu kudanganya UMMA juu ya umri wake na kumgharimu kulivua taji hilo la Miss Tanzania 2014.Ludenga amesema kuwa hali ya udanganyifu wa umri wa warembo hao huwa ni suala la kawaida na lipo kila mwaka ila kwa kuwa huwa wako makini ndiyo maana wangundua hivyo haoni sababu ya yeye na kampuni yake kuwajibika kisa Sitti Mtevu alidanganya umri. "Hashim Lundenga: sio sahihi, tupo makini na ndio maana tumegundua.


Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA