MTOTO WA MIAKA MITATU ABAKWA AFGHANISTAN



Mtoto Neelofar mwenye umri wa miaka mitatu pekee amepakatwa na nyanyake katika kiti cha nyuma cha texi ikimkimbiza hospitalini.
Ndani ya mwili wake kuna mrija ambao umaetumiwa kumpa dawa kama huduma ya kwanza kabla ya kupelekwa hospitalini.
Mkono wake mmoja umefungwa kwa bandeji ambako kuna mrija unaotumika kuingizia maji mwili mwake na ambao amewekewa akiwa hospitalini.
Mtoto Neelofar yuko katika hali mahututi, baada ya kubakwa na anahitaji matibabu ambayo anaweza kupokea tu hospitalini.
Siku chache zilizopita, Neelofar alikuwa anacheza na rafiki zake nje ya nyumba yao wakati mwanamume mmoja aliteka na kwenda naye katika shamba lililokuwa karibu na nyumba hiyo.
Kulingana na familia yake na wahukumu wa afya, mshambuliaji alimfungwa kinywa mtoto huyo na kumbaka na hata kujaribu kumuua.
Kwa karibu mtoto huyo ana majeraha mabaya na pia anahisi uchungu mwingi wakati akiendelea kupokea matibabu hospitalini.
Mwanamume huyo alimziba pua na mdomo mtoto kujaribu kumkosesha pumzi mtoto huyo kwa sababu aliogopa kwamba angepiga nduru. Mtoto huyo alikuwa ana alama nyingi shingoni mwake dalili ya majereha aliyoyapata.
Wazazi wa mtoto huyo hawakuwa nyumbani wakati wa kitendo hicho cha unyama.
Kwa bahati nzuri, familia ya mtoto hiyo inasema kuwa mwanamume aliyekuwa anapita karibu na nyumba hiyo ndiye alisikia mayowe ya mtoto huyo.
Neelofar alipatikana akivuja damu na akiwa ametupwa karibu na msikiti katika kijiji hicho.
Polisi wamemkamata mwanamume mwenye umri wa miaka 18 kuhusiana na unyama huo.
Inaarifiwa kuwa mwanamume huyo ni jirani na mtu anayejulikana kwa familia ya mtoto huyo.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA