PROF MUHONGO; FEDHA ZA ESCROW SI MALI MALI YA UMMA








Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo

Dodoma. Sakata la uchotwaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow linaendelea kuchukua sura mpya baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo kutoa ufafanuzi wa Serikali bungeni mjini Dodoma kuwa fedha hizo si za umma na kwamba bado Serikali ina mzigo wa madeni katika sakata hilo.
Kauli ya Prof Muhongo inakuja siku moja baada ya Kamati ya PAC kuwasilisha ripoti yake jana juu ya suala hilo ambapo pamoja na mambo mengine, Kamati ya PAC ilijiridhisha kuwa sehemu ya fedha hizo ni za Serikali.
Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe akisoma taarifa ya kamati hiyo jana alisema Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Francis Mwakapalila, Kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bade wakithibitisha kuwa sehemu ya fedha zilizokuwamo kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow zilikuwa za Serikali.
Akiwasilisha maelezo ya Serikali leo, Prof Muhongo alipangua hoja moja baada ya nyingine zilizotolewa na Kamati ya PAC jana na kusisitiza kuwa fedha hizo si mali ya umma.
Prof Muhongo pia alitumia muda mwingi kueleza jinsi Kampuni ya uwakili ya Mkono and Advocates iliyokuwa ikiitetea Serikali pamoja na Tanesco, ilivyochota kiasi kikubwa cha pesa kama malipo ya kazi hiyo tangu kuanza kwa mgogoro huo.
“Gharama za mawakili; Kampuni ya Mkono & Advocates waliokuwa wakiitetea Tanesco na Serikali katika suala la IPTL tangu mwaka 1998 hadi 2013 ni Sh62.90 bilioni na bado wanaidai Serikali $ milioni nne,” alismea Prof Muhongo.
Aliongeza kuwa Kampuni hiyo ya Mkono & Advocates iliishauri Serikali kuwapa kazi nyingine ya kwenda kuitetea Serikali juu ya mgogoro huo, lakini Serikali ilikataa na kuongeza kuwa waliokoa Sh95 bilioni kwa uamuzi huo kwani uwezekano wa kushinda ulikuwa mdogo.
Nchi yatikiswa
Dodoma. Hatimaye mtikisiko wa tano umetimia na nchi kutikiswa; ripoti ya Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) imependekeza kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Mwanasheria Mkuu, Waziri wa Nishati na Madini, naibu wake na katibu mkuu wa wizara hiyo wawajibishwe kutokana na kuhusika kwao kwenye sakata la uchotwaji wa Sh306 bilioni kutoka kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow.
Akaunti hiyo ilifunguliwa kwa ajili ya kutunza fedha za gharama za uwekezaji (capacity charge) baada ya kuibuka mzozo wa kimkataba baina ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na kampuni binafsi ya IPTL ambayo iliingia mkataba wa kufua umeme na kuliuzia nishati hiyo shirika hilo la umma.
Ripoti hiyo ilisomwa jana bungeni kwa kupokezana kati ya Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe na Makamu mwenyekiti, Deo Filikunjombe baada ya majadiliano marefu kwenye vikao vya ndani vya CCM na Kamati ya Uongozi wa Bunge na jitihada kubwa za kutaka isisomwe na kujadiliwa.
Ripoti hiyo ilitokana na ukaguzi uliofanywa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambayo ilianika ukiukwaji mkubwa wa taratibu wakati wa uchotaji wa fedha hizo pia mahojiano na mkurugenzi mkuu wa Takukuru na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA