MLEMAVU WA NGOZI CHUPUCHUPU KUUAWA KINYAMA HUKO TABORA





Msichana Kulwa Joseph (21) mwenye ulemavu wa ngozi (albino) mkazi wa kijiji cha usonga kata ya Sirambo wilayani Kaliua Mkoani Tabora, amenesurika kuuawa na majambazi watatu, ambapo awali walimteka Balozi wa nyumba kumi na kumpiga ili awapeleke kwa mlemavu huyo naye kwa kubaini nia mbaya akawapeleka nyumba nyingine.

Akizungumza katika kituo cha kulelea yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi cha huruma kilichoko chini ya kanisa katholiki, Binti huyo Kulwa Joseph amesema kuwa, watu ambao hawakujulikana walivamia nyumbani kwa jirani na kuanza kuwapiga mjomba wake anayeishi nyumba ya jirani.


Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Bw Saveli Maketa ambaye alimnusuru kwa kumhamisha porini walipokuwa anaishi amesema kuwa hali ya maisha ya walemavu wa ngozi wilayani humo inaonyesha kuwa hatarishi ambapo amewataka wananchi kuwa na mshikamano ili kuwanusuru na hali hiyo. 


Mratibu wa chama cha wenye ulemavu mkoani Tabora Bw, Focus Magwesera amemtaja balozi aliyejeruhiwa na majambazi hayo kwa jina la makoye meli ambapo katika kutaka kumnusuru mlemavu huyo, aliwapeleka majambazi hao kwa nyumba ya jirani, huku mwenyekiti wa walemavu wilaya ya Sirambo akitishiwa kuuawa.


Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI