MCHUNGAJI NIGERIA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUJARIBU KUTEMBEA JUU YA MAJI KAMA YESU



NIGERIA. Ilikuwa sikitisho kubwa kwa waumini baada ya mchungaji wao kusombwa na maji baada ya kujaribu kutembea juu ya maji kama vile masihi Yesu alivyofanya wakati wake alipokuwa duniani.

Pastor Frank Kabele mwenye umri wa miaka 35, aliwaambia waumini wake kuwa mtu mwenye imani anaweza kufanya miujiza yeyote ila tu uwe na imani. Aliwaahidi wafuasi wake kuwa atatembea juu ya maji pindi tu atakapomaliza maombi yake.

Lakini mambo yalienda ndivyo sivyo baada ya pastor huyo kujaribu kutembea katika mto mkubwa, alididimia mtoni humo na ilikuwa vigumu kwa waumini wake kumsaidia kwani maji yalikuwa na nguvu nyingi.

Mfuasi wa Yesu, Peter alijaribu kutembea juu ya maji kama vile Yesu alivyofanya lakini hakutoboa, alisaidiwa kuzama maji. Sasa miaka zaidi ya 2000 baadae, pastor huyu wa Nigeria alijaribu kumuiga Yesu lakini hakufaulu na majibu yake ni kuwa alipoteza maisha yake.

Ama pastor huyo aliingiwa na imani kuwa anaweza kutembea juu ya maji kama vile wale wanamazingaombwe wanavyofanya.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI