MAKONDA HAJAMPIGA WARIOBA





Makonda Hajampiga Mzee Warioba.
Makonda alikuwa anasaidia mzee asipigwe Na aliomba Msaada huo wakusaidia Pasiwe Na Mapigano mule Ndani.
Vijana wa Chadema wamewapiga sana Vijana wa CCM wamepasuka mpaka sasa Jana Usiku Saa 3 ndio nilitoka kuwatoa Hospitali kutibiwa majerehara.
Vurugu ilianzishwa Na Vijana wa CDM Kwa Kuanza Kumpiga Mama aliekuwa amekaa Mbele Kabisa alipigwa Na Kuangukia ktk Jukwaa Kuu.
Picha inayosambazwa inamuonyesha Makonda Na Warioba Na Watu kusema Kuwa Makonda Alikuwa akimpiga Mzee Sio Kweli Bali Alikuwa Akimsaidia Kutoka Nje ambapo Makonda Na Warioba walikuwa wamejificha Pale Jukwaa Kuu Baada ya Viti Kuamza Kurushwa Ukumbini Pale.
Ndugu Amon Mpanju Alikuwa akipigwa Na Wahuni wa CDM Mimi Na Makonda Tumemtetea Asiumizwe kwani Ni Mlemavu wa Macho kwani Haoni Wapi Akimbie Na Afanye nini Lakini Vijana Hawa Walinishangaza Sana Kwa Kuona Vijana Hawana Nidhamu wala Heshima Wala Huruma yakuwaonea Walemavu Huruma.
Mpanju Katangaziwa Vita pale Ukumbini kuwa watampiga yeye Na Makonda Na Vijana Wengine Na Kweli walipigwa kama Askari wasingefika Pale Kiukweli Sijui Pangekuwa Na Mauwaji gani au Majeruhi Kwa Kiasi Gani.
Picha zinaonyesha Warioba Na Makonda kama wanavutana Move ile Walipokuwa wait oka Nje Na Askari walikuwa wakimchukua Warioba Na Kumficha sehemu ambayo Askari walimlinda, Makonda, Mpanju Na Wale Watoa Mada wote waliwekwa chini ya Ukinzi.
Baada ya Mdaharo Kuhairishwa Jaji warioba aliondoka Kwa kusindikizwa Na Askari akiwa Na Wenzie.
Makonda Aliondoka akiwa Na Askari pia .
Mimi Nilibakia na Amon Mpanju Aliekuwa Mjumbe wa Bunge LA Katiba toka Kundi LA Walemavu Amon Alikuwa akitishiwa Na Alipigwa pia.
Nilibakia Pale nae Na Kuhakikisha Kaondoka Salama Nilimpandisha Gari Na Kumsindikiza Nyumbani Kwake Akiwa Salama.
Nilifatilia Makonda kapelekwa wapi Nimesikitishwa sana Na Kitendo cha Kuona Makonda Kapewa Sifa mbaya yakumpiga Mzee Warioba Na Kusema Makonda Kaleta Vurugu Ukumbini, Na Vijana Walioleta Vurugu Na Kupiga Watu Wote Hawajakamatwa Na Wala Sijawakuta Kituoni.
Kuna Vijana Walikamatwa tulifanikiwa Kuwatoa Kituoni Na Kuondoka Nyumbani Na Walioumizwa walipata Matibabu Na Kuondoka Nyumbani pia.
Kinachofanyika si Chema Kabisa Kwa Taifa letu kwani tunapanda Mbegu ya Ajabu sana Na Itatusumbua sana kama Taifa.
Yuliona Libya walianza Hivi hivi Kimasihara Kwa kuwarubuni Vijana Kufanya Mambo yakishenzi Na Kihuni Na Kupiga watu wakafanikiwa Kuitoa Serikali iliyokuwa Madarakani Kwa Mapinduzi, Kitendo kile Mpaka Leo Kinaitafuna Libya vibaya Mno.
Nchi haijatulia Na Sidhani kama Itatulia kwani Hawajui Serikali ilifikia Pale Kwa Hekima Na Busara Zipi, Walioko Libya Leo wanajuta.
Nawasowasi Na Hizi Movement zinazoanzishwa Na Viongozi wetu Nchini Tanzania.
By Peter Dafi

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI