MTOTO AFARIKI AKIWA RUMANDE NA MAMA YAKE





Mtoto mmoja amefariki dunia akiwa rumande katika kituo cha polisi KOVA pale mbezi kwa msuguli jijini dar es salaam. Tukio hili la kusikitisha sana limetokea jana wakati mama wa mtoto alipokamatwa kwa kosa linalosadikiwa kuwa ni kutolipa deni kwa wakati na alipofikishwa polisi mama huyu aliwekwa ndani akiwa amembeba mtoto wake mdogo.

Mama katika kujitetea aliwaomba askari polisi wa kituoni wamuweke ndani yeye peke yake na mtoto abaki nje ili akakae na baba yake kwani mtoto ana matatizo ya kiafya lakini polisi hawakumsikiliza na badala yake wakamsweka ndani yeye na mwanae huyo...mda mfupi baadae mtoto akafia sero!
Inasadikiwa polisi waliofanya unyama huo wamekimbia!




Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI