MCHUNGJI AKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA



Kamanda wa kikosi cha kupambana na dawa za Kulevya Godfrey Nzowa 


Jeshi la Polis kitengo cha Kupambana na Dawa za kulevya limekamata kilo40 za dawa za kulevya aina ya heroine zenye thamani ya shilingi bilioni2.
Tukio hilo lilitokea juzi eneo la Tegeta nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam ambapo Polisi walifaniikiwa kuwanasa watu wawili wakiwa na dawa hizo ndani ya nyumba inayomilikiwa na mchungaji ambaye wakati huo alikua katika kanisa lake lililopo eneo la Sinza. Kamanda wa kikosi cha kupambana na dawa za Kulevya Godfrey Nzowa alilithibitishia kuwa kuwepo kwa tukio hilo akiomba jina la mchungaji huyo lihifadhiwe kuepusha kuvuruga uchunguzi.
“Ni kweli tukio la aina hiyo lipo lakini watu kama hawa siwezi kusema moja kwa moja ni Mchungaji ndio muhusika hadi nipate vithibitisho vya kutosha ikiwa kuendesha kanisa kwani wengi wao wanatumia makanisa kama mwamvuli wa kujificha na kufanya biashara hii,”Alisema Nzowa. 

Alisema kwa sasa watu hao wanashikiliwa na Jeshi hilo ambapo wawili kati yao si raia wa hapa nchini wakati upelelezi ukiendelea kabla ya kuweka 
hadharani ukweli wa mambo.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI