DEREVA WA BODA BODA ACHINJWA



HATARI! Wimbi la mauaji yanayohusishwa na matukio ya mafumanizi yanazidi kushika kasi mkoani hapa ambapo mwishoni mwa wiki iliyopita dereva mwingine wa bodaboda aliyetajwa kwa jina moja la Kambi (33), anadaiwa kuchinjwa na kufa papohapo huku kifo chake kikihusishwa na matukio hayo.

Tukio hilo lilitokea juzikati majira ya saa 11:00 alfajiri ambapo mwili wa bodaboda huyo uliokotwa maeneo ya Modeko jirani na Makutano ya Barabara za lringa na Mazimbu na kusababisha mkewe kuchanganyikiwa huku ndugu wakiwa hawaamini.wauwaji hao hawakuchukua chochote kutoka kwa marehemu huku wakimwachia bodaboda yake na waleti ikiwa na fedha taslimu shilingi laki 240,000.

Mke wa marehemu akiwa mwenye huzuni kubwa.

             Ndugu wa marehemu Kambi.

Kufuatia hali hiyo baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo, walidai huenda jamaa huyo alifumaniwa na mke wa mtu kwani mara ya mwisho alionekana akiwa amempakiza mwanamke hivyo kuna madai kwamba mwenye mali hakuwa na sababu ya kuchukua chochote zaidi ya kumtoa roho.Majira ya saa 12:00 asubuhi, polisi walifika eneo hilo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka mochwari kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Leonard Paul.

Baada ya tukio hilo, mwanahabari wetu kusaka undani wa kifo cha bodaboda huyo. Kwenye eneo la tukio, ilidaiwa kwamba jamaa huyo aliuawa katika tukio lililohusisha fumanizi la mke wa mtu kwani baada ishu hiyo wahusika walitoka nduki bila kuchukua Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Leonard Paul alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI