MCHUNGAJI LUSEKELO AMIMINA RISASI MTAANI



NI kama kimenuka tu! Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo-Kibangu jijini Dar,  Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’ usiku wa kuamkia Jumatatu iliyopita  alizua la kuzua kufuatia kumimina risasi kadhaa hadharani kwa madai ya kuwatawanya kundi la vijana waliodaiwa kumvamia na kuziba barabara kwa lengo la kumfanyia kitu mbaya.
Ishu hiyo iliyojaa utata mkubwa, ilitokea saa nne usiku maeneo ya Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam kwenye barabara inayotoka barabara kuu kwenda kanisani kwake.
MAELEZO YA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, tukio lilianza kwa Mzee wa Upako aliyekuwa akipita kwa miguu kukejeliwa na vijana waliomwita Freemason kauli ambayo mtumishi huyo wa Mungu aliiona ni ya kejeli kwake.“Baada ya kuitwa Freemason, yule kijana akiwa na wenzake waliendelea kumkejeli Mzee wa Upako, akawafuata na kuwauliza mbona mnanitukana, nimewakosea nini?”
RISASI ZARINDIMA
“Alipoona wale vijana wanazidi kumkejeli huku wakionesha dalili za kumfanyia fujo ndipo alipotoa bastola yake na kufyatua risasi tatu juu hali iliyowafanya wale vijana kutawanyika huku na kule.
“Baadhi ya watu walikuwa kwenye biashara zao, nao walitimua mbio, wengine waliacha biashara, unajua risasi ni risasi tu, mtu akisikia risasi hawezi kukaa salama hata kama ni mjeshi,” kilisema chanzo hicho.

MZEE WA UPAKO ATIMUA MBIO
Ilizidi kudaiwa kwamba, kufuatia kimbiakimbia hiyo, Mzee wa Upako naye alikimbia. Baadaye alirudi eneo la tukio kimachale na kukuta watu wameanza kukusanyika kujua kulikoni.“Mzee wa Upako alipofika aliagiza mtu atakayeokota ‘magazini’ ya risasi alizofyatua angempa shilingi alfu ishirini, vijana wengine wakaingia kazini, wakapata moja, wakapewa chao, Mzee wa Upako akasema mtu akiokota nyingine aipeleke polisi,” kilisema chanzo.
MADAI YA WATU
Kuna madai kwamba, vurugu hizo zilipambwa na kijana mmoja anayeitwa Robert ambapo mtumishi huyo wa Mungu alimkomalia kuwa ndiye aliyekuwa akiongoza wenzake kumtukana na kumkashifu kwamba yeye ni Freemason na si mchungaji wa kiroho kama anavyojiita.
MZEE WA UPAKO NA GAZETI LA AMANI
Kufuatia madai hayo, gazeti hili lilimtafuta Mzee wa Upako kwa njia ya simu na alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, alikiri kutokea na kueleza ‘full’ mkanda.“Ni kweli lilitokea. Ni kwamba, siku hiyo nilipofika eneo lile kuna vijana wa kihuni walinifuata kwa nyuma, wakaanza kupigapiga gari langu, wengine wakizuia njia huku wakidai eti mimi ni Freemason.



Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI