YONDANI AMUONDOA TAMBWE SIMBA



                                                         
                                                Ammis Tambwe
              MASHABIKI wa Simba wanaamini kwamba timu yao ina mastraika wawili wa maana ambao ni Emmanuel Okwi wa Uganda na Amissi Tambwe wa Burundi.Lakini kocha wa timu hiyo, Patrick Phiri, akaamua kufanya uamuzi mgumu kwenye mechi dhidi ya Yanga na kuwaacha mashabiki wote midomo wa
           Phiri aliangalia kwa umakini video za Yanga kwenye mechi za kirafiki na zile za kwanza za ligi akabaini kwamba mabeki Kelvin Yondani na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wa Yanga wana nguvu sana na wanaweza kuwa na madhara, hivyo Tambwe hataweza kuwafanya chochote.Akaamua kumpiga chini Tambwe kwenye kikosi cha kwanza na kumpa nafasi Elius Maguli ambaye awali alipanga kumtumia kama ‘Super Sub’.
          Phiri ameliambia Mwanaspoti akisema: “Sikumtumia Tambwe kwenye mchezo huo kwa sababu staili yake anayocheza ni tulivu hivyo angekuwa na wakati mgumu kwa mabeki kama Yondani na Cannavaro ambao wanatumia nguvu na wababe.“Ndiyo maana nilimpanga Maguli mwenye mwili mkubwa, nguvu na kasi  ili kuwatisha mabeki hao kwenye straika acheze na Okwi ambaye ana sifa zote za straika.”
           Mzambia huyo ametoa ufafanuzi huo  kwani mashabiki wanaamini kama angemchezesha Tambwe kipindi cha pili Simba ingepata bao.Katika mchezo huo ambao ulimalizika kwa suluhu, uzoefu wa Yondani na Cannavaro ndiyo ulioifanya ngome ya Yanga kusimama imara na kutoruhusu bao ingawa muda fulani walionekana kupoteza mawasiliano.
         Maguli na Okwi walilazimisha mashambulizi na kuingia kwenye 18 bila woga jambo ambalo lilisabisha majibizano ya maneno mara kwa mara kila mmoja akitaka kumwonyesha mwenzake ni mbabe.Kuna wakati, Okwi alitaka kuwaonyesha ni zaidi yao akacheza kibabe, baada ya kumkosa, Cannavaro aliyempasia, Salum Telela na baadaye kwa Simon Msuva, alimfuata kila mmoja ambaye mpira huo ulikwenda kwake kwa nguvu ili awapokonye, lakini mwamuzi wa mchezo huo, Israel Mkongo alimwona na kumwonyesha kadi ya njano.
          Dakika ya 40 mwamuzi alipiga filimbi ya faulo kuashiria Maguli amemchezea vibaya Cannavaro, lakini straika huyo alionyesha ishara ya mwenzake kucheza kwa ulegevu.Akizungumza baada ya mchezo huo, Cannavaro alisema: “Maguli anatumia nguvu kama sisi ndiyo maana uliona kuna kazi kati yake na sisi, halafu yule ni straika na sisi mabeki lazima tumkabe asilete madhara kwetu.”


Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA