AZAM YAMNUNUA MTAALAMU WA YONDANI NA JONAS MKUDE

UKIWA na fedha na mipango hakuna kitakachokushinda. Azam FC imemnasa daktari maarufu nchini wa magonjwa ya wachezaji, Gilbert Kigadye.
Gilbert ni mtaalamu wa mifupa, ndiye amekuwa akiwatibu karibu wachezaji wote wa Ligi Kuu Bara wenye majina makubwa hasa wa Simba na Yanga pamoja na wa madaraja mengine.
Wachezaji hao hukimbilia kwa Gilbert ambako mara nyingi hujitibu kwa gharama zao wenyewe au kupewa ushauri na wanapona kabisa, baada ya hospitali mbalimbali kushindwa kuwatibu.
Sehemu ndogo tu ya wachezaji waliowahi kutibiwa na Gilbert, wa Simba ni Mkenya Raphael Kiongera ambaye yupo nje akiuguza maumivu ya goti na Jonas Mkude naye anaugulia bega. Kwa Yanga ni Jerry Tegete, Kelvin Yondani ‘Vidic’ na Mrisho Ngassa.
Mwanaspoti imemshuhudia, Gilbert katika mazoezi ya Azam yanayofanyika kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Chamanzi pamoja na kwenye mechi zao akikaa kwenye benchi la ufundi pamoja na makocha.
Ndipo likazungumza na uongozi wa Azam ambapo Katibu Mkuu, Idrissa Nassor amesema: “Tumemchukua Gilbert na atakuwa na timu kama ulivyomshuhudia kwa makubaliano maalumu.  Tutakuwa naye lakini anaendelea kufanya shughuli zake binafsi kama kawaida.Atakuwepo katika mechi zetu na kwenye mazoezi pia, tumeamua kumtumia yeye kwa ajili ya kukabiliana na majeruhi kwenye timu yetu,”alisema Nassor.
Mwanaspoti ilimtafuta Gilbert na kuzungumza naye, alisema: “Nafanya kazi na Azam kwa makubaliano maalumu, lakini naendelea na shughuli zangu binafsi kama kawaida. Lengo la kuwa nao, ninapokuwa kwenye mazoezi au mechi naangalia namna gani majeruhi yanatokea kwa wachezaji, yanasabishwa na aina ya mazoezi wanayofanya au mambo mengine pia kutibu na kusaidia mambo mbalimbali.”

                 KelvinYondan

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA