ANAYEMDHARAU JAJA HAJUI SOKA


Straika wa Yanga, Mbrazili, Geilson Santana ‘Jaja’

BEKI wa zamani wa Simba na kocha msaidizi wa Kagera Sugar, Mrage Kabange, ameibuka na kuwatolea uvivu wanaobeza kiwango cha straika wa Yanga, Mbrazili, Geilson Santana ‘Jaja’ kuwa hawajui soka la kiufundi.
Kabange ameongeza kuwa, kiufundi Jaja ni mtu hatari licha ya kauli yake kukinzana na mtazamo wa wadau ambao wamekuwa wakiponda uwezo wake tangu kuanza kwa msimu huu.
Mbrazili huyo, alitumia zaidi ya dakika 300 kabla ya kupata bao la kwanza kwenye kikosi cha Yanga, hali ambayo imewapunguza munkari mashabiki wa Yanga kumuona kama anabebwa na kocha Marcio Maximo.
 Kabange alifunguka kuwa kiufundi Jaja ni mtu wa kuogopwa na ndiye mwenye madhara katika ‘gemu’ alizomuona.
“Sijabahatika kuangalia mechi zote za Yanga, lakini Jaja ni straika hatari, ujue siyo lazima afunge yeye, angalia uwezo wa kusababisha madhara kwa timu pinzani, watu wa namna hiyo ndiyo wabaya sana, huenda akatusumbua katika mechi ijayo.
“Jaja anaweza kushindwa kufunga, lakini pasi au mazingira anayomtengenezea mfungaji, inatosha kuwapa presha wapinzani wao. Kwangu namuona ni straika hatari na anaweza kutusumbua wiki ijayo,” alisema beki huyo wa zamani wa Simba.
Yanga inatarajia kuwa mgeni wa Kagera Sugar katika Dimba la Kaitaba, Bukoba huku ikiwa na rekodi ya kuwachapa wenyeji mabao 2-1 msimu uliopita.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA