PHIRI AIFUMUA SAFU YA ULINZI, AMUINGIZA MGEVEKE

         



                                                      
                                                                          Patrick Phiri

      Katika kuhakikisha Timu yake inaibuka na ushindi katika mechi ijayo dhidi ya Stand United ya Shinyanga , Kocha mkuu wa Simba Patrick Phiri amesema kikosi chake kitabadilika kidogo na kuifumua safu ya ulinzi. Timu hiyo inatarijiwa kujitupa kwenye uwanja wa Taifa jijini  kesho jumamosi katika mechi ya Ligi kuu Bara baada ya kutoa Sare michezo miwili dhidi ya Costal Union mabao 2-2 na Polisi Morogoro 1-1.
     
     Tangu kuondoka kwa Donald Musoti, kumeonekana kuwa na tatizo katika idara ya ulinzi ambapo kwenye nafasi ya beki wa kati  kwa sasa wanaocheza ni Hassan Isihaka akisaidiana na Joseph Owino. Kocha huyo amesema kuwa amepanga kumtumia Joram Mgeveke aliyetokea Lipuli ya Iringa inayoshiriki Ligi daraja la kwanza katika mechi hiyo ya kesho. ''Tangu ameondoka Musoti safu yangu wa ulizi haipo vizuri
     
      Combination ya Musoti na Owino ilikuwa imekaa sawa ninachofanya sasa ni kujaribu kila beki kuona yupi anayefaa kucheza pamoja na Owino.Sare zimenichosha na zinaniudhi sana nimepanga kushinda mechi zote zijazo nitamtumia Mgeveke'' alisema Phiri.










Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA