COSTAL UNION, MBEYA CITY WASHIKANA UCHAWI, WAKIMBILIA TFF


                                 
                                                       MBEYA CITY  FC


                                 
                                                         COASTAL UNION FC
               
              Hali inaonekana sio shwari baina ya timu mbili kutoka mkoani Mbeya na Tanga ambapo imani za kishirikina zimetajwa kuhusika ambapo kila upande sasa umepanga kukimbilia kushitaki kwa TFF.Coastal Union waliofungwa bao 1-0 na Mbaya City katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya lakini baada ya mchezo huo Coastal wakaibuka na kusema kuwa wenyeji wao hao waliwafanyia vitendo vingi vinavyohusiana na imani za kishirikina. Mbeya City kusikia hivyo alikanusha vikali na kusema kuwa hawako tayari kudhalilishwa.
           
       Kiongozi wa msafara na mjumbe wa kamati ya utendaji ya Coastal Albert Clement Peter amesema kuwa vitendo walivyofanyiwa na Mbeya Cicty havikuwa vya Kiungwana hata kidogo hivyo wamepeleka barua yao TFF.''Walianza kufanya usiku katika Hotel tuliyofikia hata chumba cha kubadilishia nguo, uwanjani kulipigwa rangi tukashindwa kuingia tumeshapeleka barua ya kushitaki TFF'' Alisema Abert.

          Upande wa Mbeya City kupitia Afisa Habari Dismass Ten alisema ''kipigo kiliwachanganya  na ndio maana wanaanza kusingizia masuala ya Ushirikina jambo ambalo sio la kweli suala hili tutalipeleka TFF hicho wanachosema ni udhalilishaji wa wazi '' alisema Ten.


Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA