EMMANUEL OKWI AONGEZA MKATABA WA MIAKA MIWILI SIMBA



http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/2434166/highRes/818475/-/maxw/600/-/1450c9xz/-/okwi+clip.jpg

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi, ameongeza  mkataba wa kuichezea timu hiyo akisaini miaka miwili.
Awali, kiungo huyo mwenye kasi kubwa uwanjani, alisaini mkataba wa miezi sita ya kuichezea timu hiyo akitokea Yanga, akiondoka kwa mgogoro mkubwa.
Meneja wa kiungo huyo, Abdulfatah Saleh,alisema kuwa Okwi ameongeza mkataba huo baada ya kufikia makubaliano ya pande mbili kati yao na klabu hiyo.Abdulfatah alisema, awali kiungo huyo alisaini mkataba mfupi wa kuichezea Simba ili kupisha kesi iliyopo kati yake (Okwi) na Yangailiyomfungulia mashtaka kwa madai ya kukiuka makubaliano yaliyokuwepo kwenye mkataba.
Aliongeza kuwa, mara baada ya kumalizika kwa kesi hiyo iliyosimamiwa na Kamati yaSheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ndiyo akaongeza mkataba huo mwingine.
“Okwi ameongeza mkataba mwingine wa kuichezea Simba, amesaini mkataba wa miaka miwili baada ya kesi yake na Yanga kumalizika kwa TFF kumruhusu kuichezea Simba kufuatia timu ya zamani kushindwa kutimiza makubaliano yaliyokuwepo kwenye mkataba wake.

“Mwanzoni alisaini mkataba wa miezi sita ili kupisha kesi hiyo imalizike, awali alisaini mkataba huo kwa hofu ya kushindwa kesi hiyodhidi ya Yanga,” alisema Abdulfatah.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA