MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR AFUTWA KAZI

                 Aliyekuwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman

           Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi , Dk Ali Mohamed Shein, leo amemfuta kazi Mwanasheria mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman na nafasi yake kuchukuliwa na Said Hassan Said.
        Rais Shein amefanya uteuzi wa Mwanasheria mkuu wa wa Serikali ya Mapinduzi kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kufungu 55(1) cha Katiba ya Zanzibarya mwaka 1984.
      Mhe. Said Hassan Said ameteuliwa kuwa mwanasheriamkuu wa Serikali ya Zanzibar na uteuzi huo umeanza rasmi leo tarehe 7,October 2014. Kabla ya uteuzi  huo Mhe Said Hassan Said alikuwa Naibu Mwanasheria mkuu.
      Uteuzi wa Mhe. Othman Masoud Othman umefutwa kwa mujibu wa Vifungu vya 53,54(1) na 55(3) vya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na kifungu cha 12(3) cha sheria ya utumishi wa UMMA namba 2 ya 2011.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI