MTOTO WA DARASA LA TANO APEWA UJAUZITO


Mtoto anayejulikana kwa jina la Paulina (14) alitundikwa mimba na mawanafunzi mwenzake.


Mama mzazi wa Paulina, Luciana John ‘Mama Paulina’ (kushoto) akiwa na mwanaye huyo.


Mtoto mmoja aliyejulikana kwa jina la Paulina (14) mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Boko, jijini Dar amekatisha masomo kutokana na kupata ujauzito.Akizungumza kwa huzuni huku akilia, mtoto huyo alisema kwa sasa haendi shuleni kutokana na kuwa na ujauzito wa miezi miwili alioupata kwa kijana aliyemtaja kwa jina moja la Paulo mkazi wa Mbweni ambaye ni mwanafunzi wa sekondari. Alisema:
“Paulo alikuwa rafiki wa kaka yangu na alikuwa akija sana nyumbani kwetu, tukawa tumezoeana sana na siku moja akanishawishi twende kwao, tukaenda na huko ndiyo tukafanya mapenzi baada ya kuniambia atanioa nikimaliza shule.

“Alikuwa akinipa fedha mara nyingine elfu mbili au tatu ambazo nilikuwa nikizitumia shuleni, mwishowe ndiyo nikanasa,” alisema Paulina.
Akizungumza kwa huzuni mama wa mtoto huyo ambaye kazi yake ni kugonga mawe maeneo ya Chasimba, Boko, Luciana John ‘Mama Paulina’ alisema anaumia sana kwani alikuwa akitegemea mwanaye asome ili aje kumtoa kwenye shida lakini badala yake amepata mimba tena ya utotoni.
 Imeelezwa kuwa, tukio hilo limefikishwa kwenye vyombo vya sheria ili binti huyo aweze kusaidiwa.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA